Mfalme mpya wa Kuwait ameapishwa bungeni leo wakati nchi hiyo ikijitayarisha kufanya mazishi ya kiongozi wa nchi hiyo aliyefariki Sheikh Sabah al-Ahmad al-Sabah, kiongozi muhimu wa eneo la ghuba ya Uarabuni ambaye amesaidia kuwaongoza watu wake kupitia katika miongo kadhaa ya misukosuko katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Baraza la mawaziri lilimteua haraka mrithi wa mfalme, Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Sabah kuwa kiongozi jana kufuatia kifo cha Sheikh Sabah , mwenye umri wa miaka 91, ambaye mwili wake unatarajiwa kuwasili nchini Kuwait leo kutoka Marekani ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Sheikh Nawaf, mwenye umri wa miaka 83, ameahidi kufanyakazi kwa ajili ya taifa hilo mwanachama wa OPEC kuleta ufanisi, uthabiti na usalama baada ya kuapishwa kuchukua wadhifa huo.
The post Nawaf aapishwa kuwa mfalme Kuwait appeared first on Bongo5.com.