Msanii wa Bongo Movie @munalove100 leo amekutana na mama yake wa kiroho kanisani kwake kwa ajili ya kuongea na akina mama wenzake na kujaribu kuwatia moyo wale waliokata tamaa.

Akiongea na wana habari Muna ameulizwa kwanini kila anapoandaa tukio ni lazima amuongelee mtoto wake ambaye tayari ametangulia mbele ya haki Patrick na asifanye mambo mengo kwani hiyo ilikuwa mipango ya mungu.

@munalove100 amejibu kuwa ataendelea kumuongelea Patrick kwani asingekuwa Patrick huenda yeye Munah asingejulikana.

Mbali na hilo Mama wa kiroho ameongeza kuwa Munah ni jasiri sana kwani marafiki wake wote walimkataa lakini yeye aliendelea kusiamama imara hadi leo hajatetereka.