MUME wa msanii wa Bongo Muvi, Riyama Ally anayefahamika mjini kwa jina ma My Stereo, amewafokea wanaobeza penzi lake na msanii huyo aliyemzidi umri.


My Stereo alifika hatua ya kuwafokea wanaobeza penzi lao baada ya kusimangiwa jambo hilo kila kukicha akiambiwa kibenteni.


 


Kufuatia hali hiyo hivi karibuni My Stereo na baby wake huyo wakiwa wanakula minofu ndani ya kiwanja cha burudani cha Meeting Point kilichopo Kibaha Kwa Mathias, Pwani, ndipo alipoanza kuwafokea wanaolibeza penzi lao.




“Hata kama ni jimama kwani ni mama yako? Tuacheni kama tulivyo acheni kuingilia mambo ya watu,” alibwatuka My Stereo kupitia kipaza sauti kilichokuwa kwenye kiwanja hicho cha burudani.


 


Wakati jamaa akiwachana mashabiki maandazi Riyama alikuwa akirukaruka na kumshadadia mumewe wakati akiwapa makavu yao na kumwambia azidi kuwapa dozi.