Mtu mmoja ambaye hakupatikana na hatia katika shambulio la kigaidi la West Gate nchini Kenya ametekwanyara alipokuwa akielekea nyumbani.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba Liban Abdullahi Omar alikuwa ndani ya teksi na dada zake wakati watu waliojihami kwa bunduki waliposimamisha gari lao na kumtekanyara.

Wakili wake Mbugua Mureithi , aliambia Chombo cha habari cha AP kwamba watu hao walijitambulisha kama maafisa wa usalama. Polisi imekataa kutoa tamko.

Walidaiwa kumkamata na kumweka katika eneo la nyuma la gari lao mbali na kuchukua funguo za teksi hiyo.

Kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi katika mji mkuu wa Nairobi.

Omar ambaye ni mkimbizi wa Somalia nchini Kenya alikuwa anatoka katika kitengo cha maafisa wa kukabiliana na ugaidi mjini Nairobi wakati alipotekwanyara kulingana na Khelef Khalifa mkurugenzi wa shirika la haki za kibinadamu la Kiislamu Muslim For Human Rights..

Alikua ameachiliwa kutoka katika jela ya kamiti na kwamba alikuwa anajaza stakhabadhi za kumwachilia huru kama ulivyo utaratibu wa washukiwa wa ugaidi katika afisi za maafisa wa kukabiliana na ugaidi..

Watu hao walisema walikuwa maafisa wa usalama

Bwana Khalifa alisema kwamba watu waliojifunika uso waliovalia nguyo nyeusi waliizuia teksi iliokuwa imembeba bwana Omar.

Wakili wake Mbugua Mureithi aliambia runinga ya NTV kwamba watu hao wlaijitambulisha kuwa maafisa wa usalama.

Alishtakiwa pamoja na watu wengine wawili.

Wote wawili walipatikana na hatia ya kuwasaidia washukiwa wa shambulio hilo na kwamba watahukumiwa tarehe 22 mwezi Oktoba.

Ni akina nani waliohusika katika utekaji huo?

Uchambuzi wa Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi mjini Nairobi

Hakuna anayesema moja kwa moja . hakuna mtu anayetaka kukiri.

Lakini kuna makubaliano kwamba utekaji huo uliofanyika mchana huenda ulitekelezwa na watu wanaoshirikiana na kitengo cha polisi wa kukabiliana na ugaidi.

Washukiwa wengi wa ugaidi ambao wametoroka ama hata kupatikana na hatia, wametoweka ama hata kujuawa katika mauaji mabaya na watu ambao serikali haijawatambua, kuwakamata na hata kuwshtaki.

Masirika ya haki za kibinadamu yamelaumu vikosi vya usalama kwa mauaji mengi ya kiholela na kupotea kwao, huku shirika la Amnesty International mara kwlikiwakumbusha polisi kwamba hawawezi kusimamiakila kitu katika kesi .

Maafisa wa polisi mara kwa mara wamekuwa wakikana mauaji na utekajinyara

The post Mshukiwa wa shambulio la kigaidi la WestGate Kenya, atekwa na watu wasiojulikana appeared first on Bongo5.com.