Mgombea urais kupitia CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema akichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi  atahakikisha anamaliza changamoto ya ajira nchini Tanzania.


Ameeleza hayo Jumanne Oktoba 20, 2020 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mji mdogo wa Mahuta Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.


Amesema miongoni mwa ajira atakazotoa ni kuziba nafasi za watumishi wa serikali walioondolewa kwa madai ya kuwa na vyeti feki pamoja na za watumishi waliostaafu na kufariki dunia.

Amedai nafasi hizo hazijajazwa  jambo ambalo linasababisha uhaba wa watumishi katika sekta ya afya na elimu.