Mwezi Septemba 1979, aliyekuwa mfalme wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa, aling’atuliwa madarakani na nchi hiyo ikarejea katika utawala wa kiraia miaka kadhaa baada ya kushikwa mateka na mwanaume ambaye jina lake linatambulika na wengi kwenye simulizi nyingi za kushangaza. Lakini vipi kuhusu mambo yake ya ajabu ajabu?

Mwandishi wa BBC Mike Thomson anasema kwamba kwa zaidi ya miongo mitatu, jina lake limetumika kuziba ukatili na unyama mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa na madikteta enzi za baada ya ukoloni.

Historia inaonesha kwamba kwa kiasi fulani, Jean-Bedel Bokassa, au Bokassa jina alilojipa wakati alipokuwa mfalme mwaka 1977, alikuwa mmoja wa wakatili katika bara la Afrika.

Alipong’atuliwa madarakani mwaka 1976, sanamu kubwa ya mwanaume huyo aliyetawala Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa karibu miaka 14 iliwakasirisha wengi waliomchukia.

Lakini kulingana na Jean-Serge Bokassa, mmoja wa watoto wa Bokassa, wengi walikosa kumuelewa.

Anasema baba yake alikuwa mzalendo aliyefanyakazi kwa bidii kwa ajili ya nchi yake na ambaye sifa yake ilichafuliwa na wale waliotaka kumuondoa madarakani.

Jean-Serge alikuwa na miaka saba, wakati baba yake anabanduliwa madarakani.

Jean-Serge wa wengine wa familia walifurushwa na kukimbilia Gabon.

“Tuliona taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba baba yetu hadhibiti tena Jamhuri ya Afrika ya kati,” Jean-Serge alisema.

“Alimalizwa na vyombo vya habari vilivyomuelezea kama mla watu na muuaji wa watoto,” aliongeza.

“Kuna msemo unaosema ukimchukia mbwa wako, lazima useme kwamba ana ugonjwa mbaya ili uweze kumuua,” Jean-Serge anasema.

Akimaanisha kwamba waliomchukia baba yake walimuonesha kama mtu mwenye kudhuru wengine.

Fuatilia baadhi ya simulizi za ajabu za Jean-Bedel Bokassa.

“Alikula nyama ya mwanadamu.”

Bokassa ametuhumiwa kwa kula nyama ya mwanadamu, na wakosoaji wanasema kwamba alikula nyama ya waasi wake na kurusha simba na mamba ndani ya shamba lake.

Bokassa

Pia inasemekana aliagiza wezi kukatwa masikio.

Wakati wa utawala wake, Bokassa aliungwa mkono na Ufaransa, aliyekuwa koloni lake.

Mwaka 1966, Bokassa aling’atuliwa madarakani kupitia mapinduzi ya jeshi kama mkuu wa majeshi wa Jamhuri ya Afrika Kati lakini cha kushangaza alibanduliwa na rais wa Ufaransa David Dacko.

Bokassa awali alikuwa na uhusiano mzuri na aliyekuwa rais wa Ufaransa, ValĂ©ry Giscard d’Estaing, ambaye aliwahi kusema kwamba Bokassa ni rafiki yake na mmoja wa familia yake.

Lakini mwaka 1979, usaidizi kutoka kwa Ufarasa kwa Bokassa ukasitishwa.

Kile ambacho Ufaransa ilishindwa kukivumilia ni mauaji ya watoto 100 walioandama wakipinga agizo la Bokassa la kununua sare za shule kwa bei ghali kutoka kwa kampuni iliyokuwa inamilikiwa na mmoja ya wake zake 17.

Shirika la Amnesty International pia liliripoti kwamba Bokassa amehusika moja kwa moja na baadhi ya mauaji.

Utumiaji mbaya wa mali ya umma

“Kama kijana wake, kuna mambo mazuri juu yake ninayokumbuka. Baba yangu alikuwa mpenda watu, alipenda watoto wake sana na ndio sababu alizaa zaidi ya watoto 50,” Jean Serge alisema.

Lakini kuna kingine ambacho ni vigumu kusahaulika: Bokassa alitumia pesa nyingi kwa burudani, jambo ambalo lilikuwa la kipekee wakati wa utawala wake.

Bokassa wuxu dhalay caruur 50 gaadhaysa
Bokassa alizaa watoto zaidi ya watoto 50

Hakutosheka na nafasi yake kama mtawala wa muda mrefu nchini humo na akaamua kujitawaza kama mfalme na kutumia makumi ya mamilioni ya madola mali ya umma, katika sherehe kubwa iliyofanyika mji mkuu wa Bangui.

Alivaa nguo sawa na zile zilizovaliwa na mfalme wa Ufaransa Napeleon.

Aidha, alisafiri kwa gari lililokokotwa kwa farasi na kuongozwa na wanajeshi waliovaa sare sawa na zilizovaliwa na msafara wa wanajeshi wa Ufaransa karne ya 19.

Alifungwa

Baada ya kutumikia kifungo chake, Bokassa na watoto wake kadhaa waliruhusiwa kuishi uhamishoni katika majumba ya kifahari viungani mwa mji wa Ufaransa, Paris.

Lakini mwaka 1986 aliamua kurejea nyumbani na kufika huko akahukumiwa kifo na mahakama ya Afrika ya Kati bila kuwepo mahakamani, lakini baadae akaachiliwa huru na kufungwa gerezani.

Bokassa hatimae aliachiliwa kwa msamaha mwaka 1993, na miaka mitatu baadae akafariki dunia kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 75.

Khariidad muujinaysa halka Jamhuuriyadda Afrikada Dhexe kaga taal qaaradda Afrika
Khariidad muujinaysa halka Jamhuuriyadda Afrikada Dhexe kaga taal qaaradda Afrika

Baadae alirejeshewa heshima yake

Mwaka 2010, rais wa Afrika ya Kati alitoa amri ya kurejesha rasmi heshima ya Bokassa.

Azimio hilo litolewa na aliyekuwa rais Francois Bozize katika maadhimisho ya 50 ya uhuru wa nchi hiyo na kurejesha haki zote za Bokassa.

“Kurejeshwa kwa heshima ya Bokassa kunabatilisha umashtaka yote ya uhalifu ya ya Bokassa,” amri ya rais ilisema.

The post Mfahamu kiongozi wa Afrika aliyewahi kula nyama ya binadamu appeared first on Bongo5.com.