Mwanasoka mbobezi wa Uingereza anatarajia kustaafu soka baada ya kucheza mechi yake ya mwisho ya kimashindano siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 80.

Paul walking through a team guard of honour at the Paul Webster Cup in February

Peter Webster ambaye anaishi Wollongong nchini Australia amesema ametambua kwa muda sasa kuwa hatoweza kuwa na mchango kama alikuwa nao zamani hivyo amekusudia kutundika daluga .

Alianza kucheza mechi za kimashindano akiwa na umri wa miaka 15 japokuwa alisoma shule ambayo mchezo wa soka haukuwa umetawala zaidi.

Brewster alicheza timu nyingi za ligi ya Wales alipokuwa na miaka 20 na 30 kabla ya kuhamia Australia na mke wake Moira pamoja na watoto wake watatu mwaka 1981.

Nyota huyo amesema ameshangaa kuona soka la Australia limekuwa sana ”ni bora kucheza kwenye sehemu yenye joto la celsius 38 kuliko farhrenheit 38.”Peter carrying a football stands in the middle of a Webster family football team picture

Bwana Webster akiwa na wajukuu wake

Pia anatamani kuwaangalia wajukuu zake wakicheza soka katika kipindi cha ustaafu wake. Mke wake anahitaji kuona mumewake akifanya shughuli mbalimbali nyumbani.

Webster amepanga kuwasili mapema kwa ajili ya mechi ya siku ya Ijumaa usiku dhidi ya Russell Vale vinara wa ligi akiwa na timu yake ya Figtree Football hivyo anaweza kuongeza goli.Peter Webster with his son and grandson

Pia amewataka wapinzani kutambua kuwa haitokuwa rahisi hivyo wasimchukulie powa.

Bwana Webster ni gwiji ambaye anafahamika hata katika soka la mtaani na kuna mashindano ya soka yaliyopewa jina lake Peter Webster Cup.

Kuhusu mashindano hayo amesema”kwakawaida ni lazima ulipie lakini kwa mimi sitotaka kulipwa chochote na kwakuwa bado niko hai natamani sikumoja kucheza mashindano hayo”

Bwana Webster amesema amekaa muda mrefu bila kucheza na hana uhakika atajisikiaje baada ya mechi yake ya mwisho.

The post Mchezaji wa miaka 80 ajiandaa kustaafu soka appeared first on Bongo5.com.