Baadhi ya majimbo tayari washindi wametangazwa, Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Yohana Elisha, amemtangaza Saashisha Mafuwe wa CCM kuwa mshindi wa nafasi ya ubunge kwa jimbo la Hai baada ya kupata kura 89,786. Mgombea kupitia CHADEMA, Freeman Mbowe amepata kura 27,684 huku mgombea wa ACT-Wazalendo Mbaruku Mhina (ACT) akipata kura 315.
Mbali na hilo Naibu Spika @tulia.ackson ametangazwa kuwa Mshindi wa Ubunge jimbo la Mbeya Mjini. Amemshinda Joseph Mbilinyi (SUGU) wa #Chadema ambaye amekuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 10, amepata kura 75,225 akifuatiwa na Joseph Mbilinyi wa Chadema aliyepata kura 37,591.
Huku Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Moshi Mjini amemtangaza Priscus Tarimo wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 31,169, akifuatiwa na Raymond Mboya wa Chadema aliyepata kura 22,555.
Hayo yote yalikuwa majimbo yanayoshikiliwa na Upinzani yaani CHADEMA na kwa sasa yamerudi chama tawala CCM.
The post Matokeo ya Ubunge: Mbowe jimbo la Hai, Sugu jimbo la Mbeya Mjini chali, Dkt Tulia Akson kidedea appeared first on Bongo5.com.