Maelfu waandamana nchini Ufaransa kumuunga mkono Samuel Paty, mwalimu aliyekatwa kichwa kwa kuonesha wanafunzi vibonzo vya Mtume Muhammad.

Watu katika eneo la de la République mjini Paris walikuwa wameshika vipeperushi vilivyoandikwa “Je suis enseignant” (Mimi ni mwalimu), wakati waziri mkuu Castex amesema: “Sisi ni Ufaransa!”

Mwanaume mmoja anayeitwa Abdoulakh A alipigwa risasi na polisi siku ya Ijumaa baada ya kumuua bwana Paty karibu na maeneo ya shule karibu na mji wa Paris.

Watu 11 wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi.

Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu kukamatwa kwao.

Ndugu wanne wakaribu wa washukiwa walishikiliwa kwa muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Watu wengine sita walishikiliwa siku ya Jumamosi , akiwemo baba wa wanafunzi ambaye alitambulishwa na vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa alikuwa muhubiri na muislamu mwenye itikadi kali.

Rais Emmanuel Macron alisema ukatwaji wa kichwa wa mwalimu katika kitongoji kilichopo kaskazini magharibi mwa mji wa Paris -Ufaransa ni “Shambulio la ugaidi wa uislamu” na mwalimu huyo aliuawa kwa sababu alikuwa anafundisha uhuru wa kujieleza.

Mauaji hayo yanakuja baada ya shambulio la mwaka 2015 la Charlie Hebdo -ambalo lililengwa na washambuliaji kwa kuchapisha katuni za Mtume Mohammad.

Maeneo gani maandamano yamefanyika?

Eneo la de la République mjini Paris lilijaa watu wengi wakimuunga mkono bwana Paty, 47. Bwana Castex na Paris Mayor Anne Hidalgo waljumuika nao.

Makutano hayo yalijaa watu wengi wapatao milioni 1.5 wakionyesha mshikamaoni kwa Charlie Hebdo kufuatia shambulio kubwa lililotokea Januari 2015.

Muandamanaji mmoja siku ya Juapili alikuwa amebeba bango lenye maelezo “Maadui wote wa Jamuhuri hawawezi kuvumilika kabisa”,na mwingine alisema “Mimi ni profesa.Ninakufikiria wewe, Samuel.”

Undated photo of Samuel Paty
Samuel Paty, a well-liked teacher, had been threatened over showing the cartoons

Mwingine alisema Le Figaro alikuwa muislamu wa Ufaransa alielezea machungu ya mauaji hayo.

Dakika moja ya ukimya huko Marseillaise. Waandamanaji wote walikuwa wamevalia barakoa kujikinga na virusi vya corona.

Bwana Castex aliandika kwenye kurasa ya Tweeter “Hamtutishi … sisi ni Wafaransa!”

Waziri wa elimu Jean-Michel Blanquer alisema Ufaransa itafanikiwa kukabiliana na maadui wake wa demokrasia kama wataungana kwa pamoja na kwa walimu wote wa Ufaransa wanahitaji kuungwa mkono.

Nathalie, mwalimu kutoka Chelles alikuwa katika maandamano ya Paris , Le Monde ilisema alikuwa hapo kwa sababu aligundua kuwa unaweza kufa kwa kufundisha tu.

Mjini Lille, watu walikuwa wamebeba vipepperushi na mabango yaliyoandikwa “Mimi ni Samuel”.

Maelfu walikusanyika kwa pamoja eneo la Bellecour ili kutoa heshima zao za mwisho huku wengine walijitokeza mjini Nantes.

Maandamano yalifanika pia Toulouse, Strasbourg, Marseille, Bordeaux na kwingineko.

Banner in Paris

Mbali na maandamao ya Jumapili, kutakuwa na maombolezo ya kitaifa kwa ajili ya bwana Paty , siku ya Jumatano.

Jumamosi, Tareq Oubrou, imamu wa msikiti wa Bordeaux, alisema: “Mtu mstaarabu hawezi kumuua mtu asiye na hatia, huo ni ukatili.”

Tunafahamu nini kuhusu kile kilichotokea ?

People gather in Paris for Mr Paty

Mwendesha mashtaka wa masuala ya ugaidi Jean-François Ricard alisema mshukiwa alikuwa anaishi mji wa Normandy , Évreux, karibu kilomita 100 (60 miles) kutoka eneo ambalo mauaji yaitokea.

Alifika shule ambayo bwana Paty alikuwa anafundisha ,huko Conflans-Sainte-Honorine siku ya Ijumaa na kuwauliza wanafunzi wamuoneshe mwalimu huyo.

Abdoulakh A, alikuwa na miaka 18-alizaliwa Moscow lakini asili yake ni Chechen, hakuwa na uhusiano na shule hiyo au mwalimu huyo.

Alimfuata mwalimu Paty wakati akielekea nyumbani akitoka kazini.

Mwanaume aliyekuwa amebeba kisu kikubwa alimshambulia mwalimu katika mtaa wa Conflans-Sainte-Honorine, na kukata kichwa chake.

Duru za polisi zilisema walioshuhudia walimsikia mshambuliaji akisema “Allahu Akbar”, au “Mungu ni mkubwa”, kulingana na shirika la habari Reuters.

Mshambuliaji alitimua mbio, lakini polisi waliofahamishwa na umma walikimbilia katika eneo la tukio haraka.

Walipaza sauti kumwambia ajisalimishe, inasemekana aliwatishia. Polisi wakampiga risasi ambapo alikufa muda mfupi baadae.

Watu tisa, akiwemo mtoto, wamekamatwa, duru za mahama zimeviambia vyombo vya habari vya Ufaransa .

Waliokamatwa wanaripotiwa kuwa ni pamoja na ndugu wa mshambuliaji na wazazi wa mtoto anayesoma katika shule aliyekuwa akifundisha mwalimu huyo.

Teachers demonstrate outside the school after the murder of Samuel Paty
Walimu wakiwa katika maandamano

Maafisa walikabiliana na mwanaume huyo katika wilaya iliyopo karibu ya Éragny.

Uchunguzi unasemaje?

Bwana Ricard alisema bwanar Paty alikuwa amelengwa tangu aoneshe kvibonzo vya Mtume Muhammad wakati akifundisha kuhusu uhuru wa kujieleza.

Alirudia somo hilo miaka ya hivi karibuni bwana Paty, ambaye ni mwalimu wa historia na jiografia, aliwaambia wanafunzi wa kiislamu kuangalia pembeni maana wanaweza wasipendezwe.

Parents and children lay flowers outside the school after teacher Samuel Paty was beheaded

Mzazi wa mmoja wa wazazi alikasirika sana na kwenda kulalamika shuleni.

Alisindikizwa na mwanaume mmoja – Abdelhakim Sefrioui, mhubiri na mwanaharakati – ambaye alitengeneza video ya bwana Paty “voyou” na iliyotaka asimamishwe kazi.

Bwana Sefrioui aliripotiwa kujulikana na huduma ya kiintelijensia kwa miaka kadhaa.

Wote wawili wako kizimbani kwa sasa.

The post Maelfu waandamana Ufaransa baada ya mwalimu kukatwa kichwa (+Video) appeared first on Bongo5.com.