Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye alikuwa mgombea wa urais visiwani ZanzibarMaalim Seif Sharif Hamad ameachiwa kwa dhamana na sasa yuko nyumbani.

Kulingana kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe, Maalim Seif pamoja aliyekuwa mgombea mwenza pamoja na Profesa Omar Fakih wameachiwa lakini asubuhi ya leo wanatakiwa kuripoti polisi Madema saa mbili asubuhi.


Maalim Seif alikamatwa jana majira ya asubuhi kwa mara nyingine tena muda mfupi baada ya kutangaza kuongoza maandamano ya amani ili kutetea haki yao ya kidemokrasia.


Aidha, Jumanne Maalim Seif alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha mtoni Garagara na kuachiliwa saa kadhaa baadaye katika hatua ambayo ilishtumiwa vikali na viongozi wa upinzani.