Korea Kaskazini inaaminika kuwa na makombora yenye uwezo wa kupiga maeneo ya masafa marefu, ikiwemo Marekani.

Hwasong-12

Pia inadai kuwa imetengeneza bomu la haidrojeni na kuweza kuliweka kwenye kombora.

Uhusiano na Marekani na na Korea Kusini pia hivi karibuni umeshuka, baada ya Pyongyang kulipua ofisi ya uhusiano wa Kaskazini-Kusini katika eneo la mpaka.

Kifuatacho ni kile unachohitaji kujua kuhusu mpango wa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini na vikosi vyake vya jeshi.

Makombora yanayoweza kufika Marekani

Katika kipindi cha mwaka 2017, Korea Kaskazini ilijaribu makombora kadhaa kuonesha maendeleo ya haraka ya teknolojia yake ya kijeshi.

Hwasong-12 ilifikiriwa kuwa inaweza kufikia umbali wa kilomita 4,500 (maili 2,800), ikiiweka ngome ya jeshi la Marekani kwenye kisiwa cha Pacific cha Guam katika umbali mzuri wa kuipiga

Baadaye, Hwasong-14 ilionesha uwezo mkubwa zaidi huku tafiti nyingine zikionesha kwamba inaweza kusafiri hadi kilomita 10,000 ikiwa itarushwa anga za juu.

Hii ingeipa Pyongyang kombora lake la kwanza (ICBM), linaloweza kufikia New York.

Hatimaye, Hwasong-15 ilijaribiwa, ikifika umbali wa wastani wa kilomita 4,500 – mara 10 zaidi kuliko Kituo cha Anga cha Kimataifa.

Kombora likiwa limefyatuliwa linaweza kusafiri kwa umbali wa kilomita 13,000, na kuiweka kwenye shabbaha eneo la bara la nchi ya Marekani.

Hatahivyo, mashaka yanabaki ikiwa makombora haya yanaweza kufanikiwa kubeba silaha ya vita kwa umbali kama huo, na ikiwa Korea Kaskazini ina utaalam wa kufikia lengo.

Mnamo mwaka 2019, Korea Kaskazini ilifanya majaribio kadhaa ya kombora la masafa mafupi, ambayo iliongezeka mnamo Julai na Agosti kwa kile ilichokiita “maonyo” kwa Marekani na Korea Kusini kuhusu mazoezi yao ya kijeshi

Kisha mnamo mwezi Oktoba, Pyongyang ilionekana kuwa na uwezo mpya ilipojaribu kombora linaloweza kurusha kutoka kwenye nyambizi.

Kwa nadharia, kuweza kuzindua kombora lenye vifaa vya nyuklia kutoka kwenye nyambizi huongeza uwezo wa Korea Kaskazini wa kushambulia . Tishio hilo linakabiliwa na meli za zamani na ndogo za nyambizi za nchi hiyo, ambazo zinaweza kufanya safari ya kwenda moja kwa moja hadi Hawaii.

Mafanikio dhahiri ya majaribio haya yote yameibua maswali kuhusu jinsi mpango wa makombora wa Korea Kaskazini ulivyoimarika haraka sana. Waangalizi wanaamini Pyongyang inaweza kuwa imepata injini zinazofanya kazi kwa kiwango cha juu kutoka kwa mitandao haramu nchini Urusi na Ukraine.Kombora la Hwasong 14

Korea Kaskazini imeendelea na uboreshaji wa mpango wa silaha, ikizindua majaribio ya kombora mwanzoni mwa mwaka huu.

Mnamo mwezi Julai, kiongozi wake Kim Jong-un alisema Pyongyang ilitengeneza silaha za nyuklia ili kupata “nguvu”, na kuongeza kuwa nchi hiyo sasa “ina uwezo wa kujilinda”.

Mabomu ya nyuklia

Mnamo tarehe 3 Septemba 2017 Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake kubwa zaidi la nyuklia hadi sasa, katika eneo lake la majaribio la Punggye-ri.Ramani inayoonesha majaribio ya nyukilia

Idara ya Intelijensia ya jeshi la Marekani inaamini kuwa Korea Kaskazini imefanikiwa kutumia silaha ya nyukilia kutosha ndani ya kombora.

Mwezi Aprili mwaka 2018 Korea Kaskazini ilitangaza kusitisha majaribio zaidi ya nyukilia kwa sababu uwezo wake ulikuwa “umethibitishwa”.

Pyongyang pia alisema basi kwamba itaharibu vinu vyake vyote vya nyuklia.

Mamilioni ya wanajeshi

Korea Kaskazini ina moja wapo ya vikosi vikubwa ulimwenguni – ikiwa na zaidi ya wanajeshi milioni moja na wa akiba wanaokadiriwa kuwa milioni tano.

Vifaa vyake vingi ni vya zamani , lakini vikosi vyake vya kawaida bado vinaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa Korea Kusini wakati wa vita.

Korea Kaskazini pia ina karibu vikosi 200,000 maalum ambavyo vinaweza kutarajiwa kupenya Kusini iwapo kutatokea mzozo wowote.

Wanaweza kutumia mtandao wa siri-siri wa mifumo ya chini kwa chini 20-25 iliyo katika eneo la Demilitarized (DMZ) – eneo la mpaka – linaloibuka nyuma ya safu za mbele za Korea Kusini na Marekani.Majeshi

Tishio zaidi linatokana na maelfu ya vipande vya silaha za Korea Kaskazini na virusha roketi vilivyowekwa mpakani. Nguvu yake inaweza kuitikisa Korea Kusini, pamoja na mji mkuu wa Seoul, ambao uko chini ya umbali wa kilomita 60 kutoka eneo hilo

Silaha za kemikali pia zinaweza kutumika. Mnamo mwaka 2012 serikali ya Korea Kusini ilitathimini kuwa Korea Kaskazini inaweza kuwa na kati ya tani 2,500 na 5,000 za silaha za kemikali, ambayo inaweza kuwa moja wapo ya hifadhi kubwa duniani.

Vikosi vya Marekani Korea Kusini na katika eneo la ukanda

Majeshi ya Marekani yamekuwa Rasi ya Korea tangu Vita vya Korea. Leo, Korea Kusini ni ya tatu kwa kuwa na kikosi kikubwa cha jeshi la Marekani ulimwenguni.

Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Mkakati (IISS) kuna wanajeshi 28,000 wa Marekani walio Korea Kusini wakiwemo karibu wafanyikazi wa jeshi la anga 9,000. Kwa kuongezea, Marekani ina vifaru 300 vya M1 Abrams na magari ya kivita yaliyopelekwa.Silaha ya B-1B Spirit bomber ya Marekani

Washington pia imeweka mfumo wake wa mfumo wa kizuizi cha makombora ya THAAD huko Seongju huko Korea Kusini, ambaoo ungetumika kuzuia makombora ya masafa mafupi na ya kati ya Korea Kaskazini wakati wa vita.

Kikanda,Japan ina vikosi vingi vya Marekani kuliko taifa lingine lolote, na wengine 47,050 wamepelekwa, kulingana na IISS, wengi wao wakiwa wafanyikazi wa majini. Pia ina wabebaji wa ndege walio Japani.

Pia kuna vikosi muhimu vya Marekani kwenye kisiwa cha Pasifiki cha Guam, ambacho wakati mwingine huelezewa kama “mbebaji wa ndege wa kudumu”.

Korea Kaskazini hapo awali ilitishia kufyatua makombora kwenye maji karibu na Guam.

The post Korea Kaskazini na mpango wa makombora ya nyuklia yenye uwezo wa kufika Marekani  appeared first on Bongo5.com.