Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United, Edinson Cavani hajasafiri na mashetani hao wekundu kuelekea nchini Ufaransa ambapo usiku wa leo watakabiliana na PSG katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Edinson Cavani akiwa mazoezini

Cavani ambaye aliitumikia PSG kwa miaka 7 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa matajiri hao wa Ufaransa, alijiunga na Manchester United katika dirisha la majira ya kiangazi, alitarajiwa kuwakabili waajiri wake wa zamani lakini imeripotiwa kuwa hajawa timamu kwaajili ya mchezo huo.

Wachezaji wengine ambao hawatocheza katika mchezo wa leo ni pamoja na nahodha, Harry Maguire ,Mason Greenwood, na Eric Baily ambao hawapo timamu kiafya.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solksjear amemkabidhi mikoba ya unahodha kiungo Bruno Fernandes katika mchezo wa leo utakaochezwa saa nne usiku .

Ikumbukwe kocha Ole aliwatema kikosini walinzi Marcos Rojo na Phil Jones,pia mlinda mlango Sergio Romeo kwenye orodha ya wachezaji 25 wa Manchester United ambao watacheza katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya makundi.

The post Klabu bingwa barani Ulaya UEFA rasmi leo, Man United dhidi ya PSG, Cavani, Maguire kutocheza Bruno nahodha appeared first on Bongo5.com.