Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif ameachiwa baada ya kukamatwa visiwani Zanzibar.

Maalim Seif alikamatwa na maafisa wa polisi mapema leo katika kituo cha kupigia kura cha Garagara hatua ambayo imeshutumiwa vikali na viongozi wa upinzani.

Ukurasa wa twitter wa ACT -Wazalendo umeripoti kuachiwa kwa mgombea huyo wa urais visiwani humo.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Chama cha ACT Wazalendo kilisemaje hapo awali?

Hatahivyo kwa mujibu wa mtandao wa twitter wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif alikamatwa na vyombo vya dola wakati akiwa katika kituo cha kupigia kura cha Garagara.

Ruka Twitter ujumbe, 2

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Ruka Twitter ujumbe, 3

Mwisho wa Twitter ujumbe, 3

Kulingana na taarifa ya chama hicho Seif Sharrif Hamad alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha mtoni Garagara na kupelekwa katika makao makuu ya polisi kisiwani Zanzibar.

Taarifa hiyo inasema kwamba kiongozi huyo alikamatwa katika kituo hicho alipokwenda kupiga kura ya mapema baada ya vituo kufunguliwa mapema leo.

Imeongezea kusema kwamba Maalim Seif alikuwa ameapa kushiriki katika shughuli ya kupiga kura hii leo ili kuzuia kile alichokitaja kuwa 'wizi wa kura' .

Je tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC imesemaje?

Hapo jana Tume ya uchaguzi visiwani Zanzibar ZEC ilisema kwamba ni maafisa wa polisi na wale wa kusimamia uchaguzi pekee watakaoruhusiwa kupiga kura katika siku ya kwanza ya uchaguzi.

Ilisema kwamba hatua hiyo inalenga kuwapatia fursa maafisa hao ambao wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kushiriki katika chaguzi zilizopita.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Hamid Mahmod ametaja wale watakaohusika na kura hii ya mapema kuwa , Wapiga kura watakaohusika na upigaji kura mapema ni kama ifuatavyo, Wasimamizi wa uchaguzi, pili wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupiga kura, askari polisi, wajumbe wa tume, watendaji wa tume, wapiga kura wanaohusika na ulinzi na usalama siku ya uchaguzi''.

Bwana Mahmod amesisitiza kuwa wananchi hawatakiwi kwenda katika vituo vya kupiga kura isipokuwa tu kwa wale ambao orodha yao imewekwa vituoni kwa ajili ya kupiga kura ya mapema.

Aidha kulingana na utaratibu uliopo ni kwamba sio vituo vyote vitakavyofunguliwa isipokuwa tu kwa vilivyoorodheshwa kama anavyofafanunua Mmwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Hamid Mahmod.

Chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kikiongozwa na Maalim Seif kimedaiwa kuhoji uwazi kuhusu mpango wa kura hizo za mapema.

Maalim Seif amekuwa akipinga mabadiliko yanayoleta kura ya mapema akidai kwamba itasababisha wizi wa kura madai ambayo yamepingwa na tume ya uchaguzi.

Polisi haijazungumzia kuhusu kukamatwa kwake.

Historia ya uchaguzi Zanzibar

Kisiwa hicho kina historia ya uchaguzi unaogombaniwa. Uchaguzi wa mwaka 2005 ulizongwa na ghasia.

Uchaguzi wa mwisho wa 2015 ulifutiliwa mbali na mkuu wa tume ya uchaguzi kwa kutokuwa huru na haki.

Upinzani ulisusia marudio ya Uchaguzi huo na mgombea wa CCM akatawazwa mshindi.

Kuna wagombea 17 wanaowania wadhfa wa urasi kisiwani Zanzibar.

Hatahivyo ushindani mkali ni ule uliopo kati ya kiongozi wa upinzani Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye anawania kwa mara ya sita dhidi ya Hussein Mwinyi, mwana wa aliyekuwa rais wa zamani wa taifa hilo.

Rais Ali Mohammed Shein anaondoka baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

source: JUNIOR TV APP