Kijana anayefahamika kwa jina la Twaybu Omary, 22, mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amekutwa bafuni akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia waya mweusi, huku chanzo kikidaiwa ni baada ya mama yake kukataa kuwa mfuasi wa CHADEMA.

Kitanzi

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Abdi Isango amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema siku moja kabla ya kifo cha kijana huyo kulitokea tofauti ya majibizano ya kisiasa, ambapo marehemu alikuwa ni mfuasi wa CHADEMA na alikuwa akimshawishi mama yake kuhamia chama hicho ndipo mama yake ambaye ni mfuasi wa CCM akakasirika na kumpiga kofi mwanaye.

Akimzungumzia mtoto wake huyo aliyejiua, Mama mzazi wa marehemu Mariam Shamsha, amesema mtoto wake alikuwa anapenda kusoma lakini alishindwa kumtimizia ndoto zake kutokana na kipato chake kuwa kidogo.

“Mwanangu aliniambia nijiunge na CHADEMA, mimi nikakataa nikasema siwezi kujiunga, nikamuambia mimi nina uzalendo na nchi yangu”, amesimulia Mama wa marehemu.

View this post on Instagram

———————————————————————————————————————————————————Kijana anayefahamika kwa jina la Twaybu Omary, 22, mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amekutwa bafuni akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia waya mweusi, huku chanzo kikidaiwa ni baada ya mama yake kukataa kuwa mfuasi wa CHADEMA. Kitanzi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Abdi Isango amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema siku moja kabla ya kifo cha kijana huyo kulitokea tofauti ya majibizano ya kisiasa, ambapo marehemu alikuwa ni mfuasi wa CHADEMA na alikuwa akimshawishi mama yake kuhamia chama hicho ndipo mama yake ambaye ni mfuasi wa CCM akakasirika na kumpiga kofi mwanaye.  Akimzungumzia mtoto wake huyo aliyejiua, Mama mzazi wa marehemu Mariam Shamsha, amesema mtoto wake alikuwa anapenda kusoma lakini alishindwa kumtimizia ndoto zake kutokana na kipato chake kuwa kidogo. "Mwanangu aliniambia nijiunge na CHADEMA, mimi nikakataa nikasema siwezi kujiunga, nikamuambia mimi nina uzalendo na nchi yangu", amesimulia Mama wa marehemu. ( Via Eatv.tv) Written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post KATAVI: Kijana Ajiua baada ya Mama yake kukataa kuhamia CHADEMA (+Video) appeared first on Bongo5.com.