Kamati ya Maadili ya Kitaifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa taarifa ya malalamiko ya Tume hiyo pamoja na NEC kuhusu mgombea Urais kupitia Chadema, Tundu Lissu ilikabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa chama chake kwa maandishi, lakini inashangaza mgombea huyo kudai apelekewe taarifa yeye mwenyewe kitu ambacho Tume imesema ni kinyume na taratibu.


 


Hayo yamesemwa leo Jumamosi, Oktoba 3, 2020 na Katibu Kamati ya Maadili ya Kitaifa, Emmanuel Kawishe wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea sakata hilo ikiwa ni siku moja tangu Lissu asimamishwe kufanya kampeni zake kwa siku saba kwa madai ya kukiuka taratibu na kanuni za uchaguzi.


 


“Kwa kuzingatia taratibu, Tume hupeleka taarifa kwa Katibu wa chama husika kuhusu tarehe ya kuchukua fomu na kurudisha, Tume haimpelekei taarifa mgombea mmoja mmoja, Tume inawasiliana na Katibu Mkuu na si vinginevyo.


“Madai ya Lissu kwamba hajapokea taarifa ya malalamiko mpaka leo ni uongo, chama chake kilipokea taarifa ya malalamiko kutoka Tume ikimtaja kwa jina lake yeye mwenyewe, barua ilielekezwa kwa katibu mkuu wa chadema sababu ndiye aliyemdhamini na kumtambulisha kuwa Lissu ndiye mwanachama na mgombea wa kiti cha rais kupitia chadema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.


 


“Kamati ilifikia uamuzi baada ya majadiliano baina ya walalamikaji na wawakilishi wa Chadema, alipewa taarifa na haki ya kusikilizwa, adhabu inatakiwa kutekelezwa na aheshimu adhabu hiyo, kamati si Tume bali chombo kinachoundwa na vyama ikiwemo Chadema.” -Emmanuel Kawishe, Katibu Kamati ya Maadili ya Kitaifa.

” -Emmanuel Kawishe, Katibu Kamati ya Maadili ya Kitaifa