Mwanariadha wa Uganda Joshua Cheptegei alivunja rekodi ya dunia upande wa wanaume katika mbio za mita 10,000 huku mwanariadha wa Ethiopia Letesenbet Giedy akivunja rekodi ya wanawake katika mbio za mita 5000 mjini valencia nchini Uhispania.

Cheptegei mwenye umri wa miaka 24 aliweka muda wa dakika 26 na sekunde 11 na kuvunja rekodi ya miaka 15 iliowekwa na mwanariadha wa Ethiopia Kenenisa Bekele kwa zaidi ya sekunde sita.Gidey alivunja rekodi ya dunia ya miaka 12

Image caption: Gidey alivunja rekodi ya dunia ya miaka 12

Gidey mwenye umri wa miaka 22 aliweka muda wa dakika 14 na sekunde 6.62 na kuvunja rekodi iliowekwa na Tirunesh Dibaba 2008.

Walifikia muda huo katika mbioa za NN Valencia za rekodi za dunia.

Nafurahia alisema Gidey ambaye alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 kwenye mashindano ya riadha ya dunia mjini Doha Qatar 2019.

‘’Hii imekuwa ndoto ya muda mrefu. Ni kitu kikubwa kwangu. Rekodi ya Bekele ya awali ya muda wa dakika 26 na sekunde 17 .53 ilisimama kwa muda mrefu bila kuvunjwa’’.

Joshua Cheptegei and Letesenbet Gidey break world records in Valencia | Athletics News | Sky Sports

Rekodi ya awali ya Bekele ya dakika 26 na sekunde 17.53 ilikuwa ndio ya muda mrefu zaidi kudumu katika historia kwa mbio za mita 10,000 kwa wanaume.

Mafanikio ya Cheptegei yanaadhimisha rekodi ya nne duniani katika kipindi cha miezi 10, baada ya kuvunja rekodi ya mbio za marathoni ya kilomita 10 Desemba na kilomita 5 mwezi Februari.

Katika mbio za Monaco Diamond League zilizofanyika Agosti, alivunja rekodi nyingine ya dunia ya Bekele, ya miaka 16 ya mita 5,000 kwa sekunde mbili.

The post Joshua Cheptegei wa Uganda avunja rekodi ya Dunia Hispania appeared first on Bongo5.com.