Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amewataka wananchi baada ya kupiga kura hapo kesho warejee nyumbani badala ya kukaa katika eneo hilo kwakuwa wenye jukumu la kulinda kura ni mawakala.

”Jana Oktoba 27, 2020 usiku, Pemba wakati tunasambaza masanduku ya kupigia kura walianza kurusha mawe, kwahiyo hatutarajii hayo kujirudia kama unajua hutopiga kura usiwe sehemu ya kuanzisha vurugu” – IGP Sirro

”Kuna maisha baada ya Uchaguzi, tujihadhari na mihemko isiyokuwa na tija kwa taifa kila mmoja anategemewa na familia yake usipeleke matatizo kwa familia yako” – IGP Sirro

“Sisi kama Jeshi la Polisi tutahakikisha kwamba tunatenda haki, kuhakikisha kwamba yule ambaye atachaguliwa na wananchi ndiye atakayekuwa kiongozi”.IGP Sirro.

Video bofya HAPA

The post Jeshi la polisi tutahakikisha tunatenda haki – IGP Sirro appeared first on Bongo5.com.