Wanasema ukitaka kufanikiwa kwenye biashara, fanya ile ambayo inahusisha hobby yako. Kwamba kama unapenda fashion, fanya biashara ya mavazi au urembo, na vipi kama unapenda bangi kama Jay Z Mule mule!

Rapper huyo ambaye ni baba wa watoto watatu, jana Ijumaa Oktoba 23, ameitambulisha rasmi brand yake mpya ya Bangi iliyopewa jina 'Monogram', pamoja na kutambulisha tovuti na ukurasa rasmi wa Instagram kwa ajili ya Brand hiyo.


Mbali na JayZ, pia wapo marapper wengine ambao wanafanya biashara ya kuuza bangi, ambao ni Snoop Dogg, 2 Chainz, Wiz Khalifa, Rick Ross, A$AP Rocky, Xzibit, Sojaboy, The Game, J uicy J na Waka Flocka ikiwa wao wlishaingia kwenye biashara hiyo ya Bangi kwa muda sasa.