Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amesema kuwa wamejipanga kulinda amani katika kipindi zoezi la upigaji kura kwenye uchaguzi Mkuu huku akitaja sababu kwanini wameweka askari wakutosha mkoani Arusha.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Arusha, Sirro amewaambia wananchi kuwa askari wamejipanga kuhakikisha wanasimamia amani na haki.

“Arusha ni mahala ambapo miaka ya nyuma kulitokea fujo kwahiyo ni mahala ambapo tumepanga, tumeweka askari wa kutosha, askari wa kirai, wa operesheni na askari wa upepelezi wote wapo timamu kuhakikisha arusha inakuwa shwari” amesema IGP Sirro

Aidha IGP Sirro ametoa tahadhari kwa vikundi mkoani humo ambavyo vinataka kuleta uvunjifu wa amani kulekea uchaguzi mkuu, “Nina taarifa kuna vikundi vichache vinataka kuleta uvunjifu wa amani wasijaribu kufanya hivyo wakifanya hivyo maana yake wanajiingiza kwenye kutenda makosa natutawashugulikia kabla ya siku yenyewe” amesema IGP Sirro.

https://bit.ly/2TqFxGQ

The post IGP Sirro avionya vikundi vitakavyofanya vurugu Arusha siku ya Uchaguzi (+Video) appeared first on Bongo5.com.