Marekani inatekeleza hukumu ya kifo kwa mfungwa wa kike kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka 70, kulingana na Wizara ya Sheria.

Lisa Montgomery alimyonga mwanamke mjamzito huko Missouri kabla ya kumkata mama huyo tumbo lake na kumtoa mtoto aliyekuwa amembeba mwaka 2004.

Anatarajiwa kuchomwa au kudungwa sindano ya sumu Desemba 8.

Mwanamke wa mwisho kuhukumiwa kifo na serikali ya Marekani alikuwa Bonnie Heady, aliyekufariki dunia kwenye chumba cha gesi huko Missouri mwaka 1953, kulingana na kituo cha taarifa za adhabu ya kifo.

Hukumu ya serikali dhidi ya Brandon Bernard, ambaye pamoja na washirika wake waliwauwa mawaziri wawili vijana mwaka 1999, pia imepangiwa kutolewa Desemba.

Mwanasheria mkuu William Barr alisema uhalifu huo “ni vitendo vya kinyama”.

Mwaka jana, utawala wa Trump ulisema kuwa utaanza tena kutekeleza hukumu ya kifo.

 

Lisa Montgomery ni nani?

Desemba 2004, Montgomery alisafiri kutoka Kansas hadi nyumbani kwa Bobbie Jo Stinnett, huko Missouri, kwa madai kwamba ameenda kununua mbwa, kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Sheria.

“Wakiwa ndani ya makaazi, Montgomery alimshambulia na kumnyonga Bi. Stinnett – aliyekuwa na ujauzito wa miezi nane – hadi mwathirika akapoteza fahamu,” taarifa iliyotolewa inasema.

“Kwa kutumia kisu cha jikoni, Montgomery alikata tumbo la Bi. Stinnett kulikosababisha arejeshe fahamu. Wakaanza kukabiliana na Montgomery akamnyonga Stinnett hadi akafariki dunia. Kisha, Montgomery akamtoa mtoto aliyekuwa kwenye tumbo la Stinnett, na kumchukua mtoto huyo akijaribu kujifanya kuwa ni wake.”

Mwaka 2007, jopo lilimpata Montgomery na hatia ya kuteka nyara kulikosababisha kifo kulingana na sheria za serikali nchini Marekani, na kwa kauli moja wakapitisha hukumu ya kifo dhidi ya mtuhumiwa.

Hata hivyo wakili wa Montgomery wanasema ubongo wa mteja wake uliathirika kwasababu ya kichapo alichopigwa akiwa mtoto hivyobasi hayuko sawa kiakili na kutokana na hilo mteja wake hastahili kuhumiwa kifo.

Hukumu ya kifo ilipigwa marufuku katika ngazi ya majimbo na serikali kuu kulingana na uamuzi ulitolewa na mahakama ya juu zaidi mwaka 1972 iliyofuta hukumu zote za kifo zilizokuwa zimetolewa kufikia wakati huo zikifutwa.

Aidha mwaka 1976 mahakama ya juu zaidi Marekani iliruhusu majimbo kurejesha tena hukumu ya kifo na mwaka 1988 serikali ikapitisha sheria iliyoruhusu tena utekelezaji wa adhabu hiyo kwa ngazi ya serikali kuu.

Kulingana na takwimu za Kituo cha taarifa za hukumu ya kifo, watu 78 walihukumiwa kifo katika ngazi ya serikali kuu kati ya mwaka 1988 na 2018 lakini ni watatu tu waliotekelezewa hukumu hiyo.

Hukumu ya of Montgomery na Bernard zitakuwa za nane na tisa ambazo serikali kuu ya Marekani imetekeleza mwaka huu.

Kwanini hukumu hiyo inaanza kutekelezwa tena sasa?

Kwanini hukumu hiyo inaanza kutekelezwa tena sasa?

Mwaka jana utawala wa Trump ulisema kuwa utaanza tena kutekeleza hukumu ya kifo baada ya kusitishwa kwa muda mrefu.

Taarifa iliyotolewa wakati huo, mkuu wa sheria alisema: “Chini ya utawala wa vyama vyote, wizara ya sheria imeamua kutekeleza tena hukumu ya kifo kwa wanaotekeleza uhalifu mbaya zaidi.

“Wizara ya sheria inaunga mkono sheria hiyo – na waathirika na familia zao wanatudai tuendelee kuitekeleza sheria iliowekwa na mfumo wetu wa haki.

View this post on Instagram

—————————————————————————————————————————————–Marekani inatekeleza hukumu ya kifo kwa mfungwa wa kike kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka 70, kulingana na Wizara ya Sheria. Lisa Montgomery alimyonga mwanamke mjamzito huko Missouri kabla ya kumkata mama huyo tumbo lake na kumtoa mtoto aliyekuwa amembeba mwaka 2004. Anatarajiwa kuchomwa au kudungwa sindano ya sumu Desemba 8. Mwanamke wa mwisho kuhukumiwa kifo na serikali ya Marekani alikuwa Bonnie Heady, aliyekufariki dunia kwenye chumba cha gesi huko Missouri mwaka 1953, kulingana na kituo cha taarifa za adhabu ya kifo. Hukumu ya serikali dhidi ya Brandon Bernard, ambaye pamoja na washirika wake waliwauwa mawaziri wawili vijana mwaka 1999, pia imepangiwa kutolewa Desemba. Mwanasheria mkuu William Barr alisema uhalifu huo "ni vitendo vya kinyama". Mwaka jana, utawala wa Trump ulisema kuwa utaanza tena kutekeleza hukumu ya kifo. Lisa Montgomery ni nani? Desemba 2004, Montgomery alisafiri kutoka Kansas hadi nyumbani kwa Bobbie Jo Stinnett, huko Missouri, kwa madai kwamba ameenda kununua mbwa, kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Sheria. "Wakiwa ndani ya makaazi, Montgomery alimshambulia na kumnyonga Bi. Stinnett – aliyekuwa na ujauzito wa miezi nane – hadi mwathirika akapoteza fahamu," taarifa iliyotolewa inasema. "Kwa kutumia kisu cha jikoni, Montgomery alikata tumbo la Bi. Stinnett kulikosababisha arejeshe fahamu. Wakaanza kukabiliana na Montgomery akamnyonga Stinnett hadi akafariki dunia. Kisha, Montgomery akamtoa mtoto aliyekuwa kwenye tumbo la Stinnett, na kumchukua mtoto huyo akijaribu kujifanya kuwa ni wake." Mwaka 2007, jopo lilimpata Montgomery na hatia ya kuteka nyara kulikosababisha kifo kulingana na sheria za serikali nchini Marekani, na kwa kauli moja wakapitisha hukumu ya kifo dhidi ya mtuhumiwa. Hata hivyo wakili wa Montgomery wanasema ubongo wa mteja wake uliathirika kwasababu ya kichapo alichopigwa akiwa mtoto hivyobasi hayuko sawa kiakili na kutokana na hilo mteja wake hastahili kuhumiwa kifo. (Via B.C Begley) Written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Huyu ndio mwanamke wa kwanza Marekani kuhukumiwa kifo tangu 1953 (+Video) appeared first on Bongo5.com.