Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Kigoma Mjini amemtangaza Kirumbe Ng’enda wa CCM kuwa Mshindi wa Ubunge wa Jimbo hilo kwa kupata kura 27,638 akifuatiwa na aliyekuwa Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo aliyepata kura 20,600.


Akizungumzia matokeo hayo, Zitto Kabwe amesema; “Licha ya kuingiza kwenye vituo kura zilizokwishapigwa zipatazo 15,850 (kura 50 kila Kituo cha kupigia kura)nimemshinda Mgombea wa CCM kwa kura 5218. Hata hivyo Mgombea wa CCM katangazwa mshindi kwa tofauti ya kura 7000.”