Matokeo ya uchaguzi mkuu Tanzania bado yanaendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo. Kwa mujibu wa Tume hiyo asilimia 60 ya matokeo ya urais yameshatangazwa huku katika majimbo zaidi ya 150 yaliyotufikia baada ya kutangazwa na tume, ni majimbo mawili tu yamechukuliwa na upinzani mpaka sasa, huku majimbo yaliyotazamwa kama ngome ya upinzani kwa miaka mingi, yakinyakuliwa na chama tawala, cha CCM.

Mbunge mmojawapo wa upinzani aliyetangazwa kushinda ni Shemsia Mtamba, wa Mtwara vijijini aliyemshinda Hawa Ghasia, mmoja wa vigogo na aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya Taznania kwa vipindi tofauti.

Wabunge wa Upinzania waliofanikiwa kushind amajimbo yao.

Aidah Kenani.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nkasi Kaskazini Kwangura Misana, amemtangaza Aidah Kenani wa CHADEMA kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo, baada ya kuibuka na ushindi wa kura 21,226 baada ya kumshinda Ally Keissy wa CCM aliyepata kura 19,972.

Shamsia Mtamba.

Shamsia Mtamba wa Chama cha Wananchi (CUF) ametangazwa kuwa Mbunge wa Mtwara vijininj baada ya kupata kura 26,262 mbele ya Hawa Ghasia wa #CCM aliyepata kura 18,505.

 

 

The post Hawa ndio Wabunge wawili wa upinzani Tanzania, walioshinda majimbo yao mpaka hivi sasa appeared first on Bongo5.com.