Klabu ya Simba imewataja wachezaji wake wa kimataifa ambao wameitwa kwenye timu zao za Taifa ambazo wikiendi ijayo zitacheza michezo ya kirafiki.


Wachezaji wenyewe ni Francis Kahata na Joash Onyango ambapo wawili hao wanaichezea timu moja ambayo ni Harambee Stars ya Kenya, Luis Miquissone yeye anacheza ndani ya timu ya Taifa ya Mozambique na mchezaji mwengine ni Clotous Chama yeye anacheza timu ya taifa ya Zambia.