Hamisa Mobetto Avujisha SIRI Kubwa 'Nilipata Mimba Tatu za Diamond Platnumz Lakini Zote Zikaharibika


Kwa Mara ya Kwanza kabisa kupitia Kipindi cha The Switch cha @wasafifm , Mwanamuziki na Mjasiriamali hamisamobetto amethibitisha kuwa kabla ya Kumzaa Dylan , alishabeba ujauzito wa Diamond Platnumz mara 3 Lakini ukaharibika bahati mbaya .

Hamisa amesema hayo baada ya kuulizwa kuwa Je , Diamond alishawahi kutaka kupima DNA ili kuthibitisha kuwa Dylan ni Mtoto wake ; ?

Akijibu swali hilo Hamisa amesema : “. Nadhani katika Mtu mwenye uhakika zaidi kuhusu Mtoto kuwa ni wake au sio wake ni Diamond, kwasababu hata kabla sijapata mimba ya Dylan , nilishapata ujauzito wake mara 3 na bahati mbaya ukaharibika” - hamisamobetto