Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya TUJUZANE

Android ===> GooglePlay 


Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye sasa ni Meneja wa Kampeni wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe, Josephat Gwajima akizungumza kwenye mkutano huo.


WAGOMBEA Ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo la Kawe na Kinondoni leo, wametoa tathimini ya kampeni walizopiga na jinsi walivyowafikia wananchi na kubaini ushindi wa kishindo wanaotarajia kuupata katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.Gwajima akizungumza kwenye mkutano huo leo.


Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari jijini Dar, leo Gwajima ambaye alikuwa na Meneja wake wa Kampeni, Benjamini Sitta amesema kwa kampeni aliyofanya jimboni humo kwa mikutano ya hadhara na kuwafikia wananchi nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa kijiwe kwa kijiwe na kushuhudia kero wanazokumbana nazo wananchi wa jimbo hilo na kumfikishia Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye naye amemuahidi kumsaidia kuzitatua ni ishara tosha ya ushindi wake wa kishindo.Mkutano huo ukiendelea.


Naye Meneja wa Kampeni wa mgombea wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia, aliyemuwakilisha mgombea Abbas Tarimba alisema kutokana na umahiri wa mgombea huyo na kampeni walizopiga wanatarajia kupata ushindi wa kishindo.Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia ambaye sasa ni Meneja wa Kampeni wa mgombea ubunge jimbo hilo, Abbas Tarimba akionesha kitabu chenye tathmini waliyofanya.


Mtulia amesema mgombea urais kupitia chama hicho Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mengi kwenye jimbo hilo na kuahidi kujenga Flyover nyingine tatu kwenye jimbo hilo hivyo wananchi hawana budi kumchagua na mbunge hilo ili aungane na rais kuharakisha maendeleo hayo.


“Rais wetu ametuahidi flyover zingine tatu kwenye jimbo letu Magomeni, Mwenge na Morocco ili kupunguza msongamano, sasa kwa yote hayo ni kwanini wananchi wasimpe kura na mbunge wa jimbo hilo ili kuboresha na maengineyo”. Alisema Mtulia ambaye msimu uliopita ndiye aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.   HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL