Kiungo na nahodha wa zamani wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi raia wa Congo DR amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumia club ya AS Vita ya Congo DR.

 

Tshishimbi amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa club Bestine Kazadi na sasa yupo tayari kuanza kuitumikia timu hiyo baada kuonekana mara kadhaa akifanya nao mazoezi.

 

Hata hivyo Tshishimbi anasaini na AS Vita kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga na kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mwingine.