Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi amewahidi Wazanzibar kuwa serikali yake ikingia madarakani  itahakisha bandari mpya ya mafuta na gesi itajengwa eneo la Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Dkt.Hussein Mwinyi ametoa ahadi hiyo alipokuwa akizumgumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi na wakazi wa Bumbwini Mkoa Wa Kaskazini Unguja Oktoba 07, 2020 na kusema mradi huo umeshaanza na utakamilishwa na serikali yake.
 
Aidha, amesema atavipa kipaumbele vikundi vya ujasiriamali kwa kuvipatia mikopo na mafunzo ili wanufaike na fursa hizo. Aidha, alisema atahakikisha wananchi wa wilaya hiyo wananufaika na ufugaji wa kisasa wa samaki ili waende sambamba na dhana ya uchumi.

Pia amejiombea kura na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM ili CCM iendelee kuongoza dola. Pamoja na hayo, aliwataka wananchi walinde amani ya nchi na wasikubali kuchokozeka na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wapinzani