Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya TUJUZANE
Android ===> GooglePlay
MSANII wa bongo Fleva na Mmiliki wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Nasib Abdul ‘Diamond’ ambaye mwanzoni mwa mwaka alitambulishwa kama Balozi wa kampuni ya rangi ijulikanayo kama Coral Paints ameahidi tena kufanya mambo makubwa kwa wananchi wenye kipato cha chini kwa kusaidia kuboresha makazi na nyumba zaidi 100 za familia tofauti tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam nyumbani kwa mama yake Madale, Diamond kwa kushirikiana na uongozi wa kampuni hiyo, wameahidi kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini ambao hawajaweza kumalizia ujenzi wa nyumba zao.
Alisema mpango huo unalenga kuwasaidia wananchi hao kupaka rangi nyumba zao ziwe katika muonekano mzuri. “Unajua nyumba zetu za uswahilini na kule kwa wenzetu washua hazina tofauti ila wanapotupiga bao ni katika umaliziaji , uchaguzi wa rangi wanaoufanya na mbwembwe tu na tumegundua kuwa hizi nyumba za uswahilini tunazoziona nyingi ni nzuri ila zimekosa rangi na umaliziaji mzuri tu”
“Kuanzia siku hii ya leo sisi kama Coral Paints kulidhihirisha hilo kwa ndugu zetu, watanzania wenzetu, mikoa na mitaa mbalimbali tutafi kia nyumba zaidi ya 100 tutakuwa tunawafanyia fi nishing ya nyumba zao kwa kuwapakia rangi mbalimbali na ni bure hawatochangia ela yoyote” alisema.