Klabu ya Manchester United imetangaza kupata hasara ya pauni milion 70 zaidi ya bilion 211 za kitanzania, katika mapato yake ya mwaka ikiwa ni sehemu ya athari za Covid-19.


Mapato ya Manchester United yameshuka kwa asilimia 20 ukilinganisha na mwaka wa fedha uliopita.


Mapato ya Man United kwa mwaka wa fedha wa 2019-20 ambao ukomo wake ulikuwa mwezi Juni 2020, umekuwa ni mwaka ambao wamekusanya kiwango cha chini cha mapato tangu mwaka wa fedha wa 2014-15 ambao walikusanya pauni milion 395.2 zaidi ya Trilioni 1 kwa fedha za kitanzania.


Mapato kwa ujumla ya Manchester united kwa mwaka wa fedha wa 2029-20 ni pauni million 509, zaidi ya Trilioni 1.5 kwa pesa za kitanzania, ikiwa ni mporomoko wa asilimia 18 ukilinganisha na msimu uliopita ambapo walikusanya pauni million 627.1 sawa na Trilioni 1.9.


katika mchanganuo huo unaonyesha pesa za haki za matangazo ya televisheni imeshuka kwa asilimia 41.9, kutoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita ni moja ya sababu mapato ya televisheni kushuka.


Lakini pia mapato yaliyokuwa yanapatikana siku za michezo yamepungua kwa asilimia 19  kutokana na michezo kuchezwa pasipo na uwepo wa mashabiki toka mwezi Machi.