Kiungo  wa Ujerumani, Mesut Ozil hatakuwepo kwenye kikosi cha Arsenal cha Europa kinachotarajiwa kutangazwa leo na Kocha Mikel Arteta. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hajaichezea The Gunners tangu Machi mwaka huu na hatma yake klabuni hapo imekuwa mashakani kwa muda mrefu .

Ozil, ni mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika historia ya Arsenal, alicheza katika kila mchezo wa Ligi Kuu chini ya Arteta hadi msimu uliposimamishwa kwa sababu ya janga la Corona na hajaonekana tangu hapo.

Alipoulizwa hivi karibuni kwanini mshindi wa Kombe la Dunia alikuwa amepoteza nafasi Arteta alijibu: “Timu inabadilika, unaweza kuona kiwango wanachofikia . “Hapa ndipo tulipo kwa sasa. Tunataka kubadilika zaidi na kucheza vizuri na kushindana vizuri.

“Tunahitaji kuendelea kudumisha hali hiyo. Nina furaha sana na utendaji hapa, kwa kinachoonyeshwa na wachezaji inaniwia ugumu kuchagua kikosi pia si rahisi Ozil kupata nafasi” .

Siku ya Jumanne, Ozil alijitolea kulipa mshahara kamili wa Jerry Quy ambaye anavaa kinyago kinachohamasisha mashabiki wa The Gunners kwa miaka 27 iliyopita na hivi karibuni alitangaziwa kusitishiwa huduma yake kutokana na kuporomoka kiuchumi kwa klabu hiyo.

Kampeni ya Ligi ya Uropa ya Arsenal itaanza wakati watakapomenyana na wapinzani wa Kundi B Rapid Vienna huko Austria mnamo Oktoba 22 kabla ya mechi dhidi ya Dundalk na Molde

The post Bundi aendelea kuyaandama maisha ya soka ya Ozil, atemwa kwenye kikosi cha Arsenal Europa appeared first on Bongo5.com.