Msanii wa RnB Bongo Ben Pol ameweza ameshtua wengi baada ya kubadilisha dini na kuhamia kwenye uislam ambapo amepost picha akiwa amevaa kanzu katika msikiti wa Maamur uliopo maeneo ya Upanga Jijini Dar Es Salaam chini ya Imam Mkuu wa msikiti huo Sheikh Issa Othman Issa.

Msanii Ben Pol na cheti chake baada ya kubadilisha dini

Kupitia picha hiyo Ben Pol ameandika kuwa “Bismillah-hir-rahman-nir-rahim 23.10.2020” kisha akaweka alama za kushukuru.

Aidha ukipitia kwenye Insta Stori yake ameshea picha ya cheti chake ambacho kinaonyesha maandishi ya kubadilisha kutoka kwenye uikristo hadi kuwa muislam ambapo jina lake jipya ni Benham Paul Mnyanganga baada ya lile jina lake la zamani Benard Paul Mnyanganga.

Hizi hapa ni comments za baadhi ya mastaa wenziye wakimpongeza baada ya kubadilisha dini

“Mabrook Mabrook” – Ommy Dimpoz

“Umeamua kujikuta Tyrese sio” – Fid Q

“Mashallah, Alhamdulillah” – Mwana Fa

“MashAllah Jina tu hujasema Shekhe” – Dullah Planet

Tumejaribu kumtafuta Ben Pol ili aweze kufafanua zaidi kuhusu chanzo cha kubadilisha dini lakini kwa bahati mbaya hakushika simu yake, pia tumemtafuta Imam Mkuu wa Msikiti huo lakini na yeye hatukumpata hewani.

The post Ben Pol abadilisha dini ataja jina lake la Kiislam, Mastaa mbalimbali wampongeza appeared first on Bongo5.com.