Waziri wa Elimu wa Kenya George Magoha kwa mara nyikingine tena amesema shule zinastahili kufunguliwa sasa na wala sio mwezi Januari mwaka ujao.
Akizungumza na kamati ya bunge kuhusu elimu suku ya Jumanne Bw. Magoha alisema hata kama serikali itasubiri hadi Januari mwaka 2021, mwenendo wa ugonjwa wa Covid -19 huenda isibadilike akiongeza kuwa watoto wapo salama zaidi shuleni kuliko nyumbani.
“Lazima tufanye maamuzi magumu.Wakati wa kufungua shule ni sasa,” Waziri Magoha aliiambia kamati ya bunge.
Amesema wizara yake inafanya kazi na wahika dau wa sekta ya elimukujadili “jinsi” shule zitakavyofunguliwa“hivi karibuni ”, huku akifuchua kuwa mapendekezo yaliyotolewa na jopokazi la elimu kuhusu mweneno wa Covid 19 ilijumuisha changamoto zote zinazokabili ufunguzi wa shule wakati huu wa janga la corona.
Jopokazi hilo lilikuwa limependekeza shule za msingi na za upili kufunguliwakati ya tarehe 5 na 19 Oktoba 2020. Alisema kalenda hiyo mpya ya ufunguzi wa shule ilikuwa imepangwa njia ambayo ingehakikisha hakuna mtoto angerudia darasa.
The post Baada ya Corona kuisumbua sana Kenya, sasa Shule ruksa kufunguliwa (+Video) appeared first on Bongo5.com.