Aston Villa inajiandaa kuwauza winga wake mdachi Anwar El Ghazi, 25, beki mfaransa Frederic Guilbert, 25, na kiungo wao Muingerereza, Henri Lansbury, 29, kabla dirisha la usajili wa ndani kufungwa Oktoba 16.

Villa inafanya hivyo ili kupunguza gharama za kikosi hicho wakijiandaa kumsainisha mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28, ambaye anawaniwa pia na West Ham. (Football Insider)

Manchester City itaweza kumsajili kiungo mchezeshaji kutoka Barcelona, Muargentina Lionel Messi, 33, msimu ujao kama fursa hiyo itajitokeza, anasema Afisa mkuu uendeshaji Omar Berrada. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, raia wa Norway striker Erling Haaland, 20, na winga wa klabu hiyo, kutoka England Jadon Sancho, 20, bado wako kwenye orodha kuu ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya Manchester United. (ESPN)

Real Madrid imeoondoa uwezekano wa kumsajili kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, baada ya kusema ilikuwa ndoto yake kuchezea klabu hiyo siku moja. (AS – in Spanish)Kelvin

Kiungo wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 29, anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka miwili wenye thamani ya £300,000 kwa wiki kusalia Manchester City. (Sun)

Beki wa Arsenal’s aliyesajiliwa kwa £27m Mfaransa William Saliba, ambaye hajacheza mchezo wowote wa ligi msimu huu, anajiandaa kucheza Championship kwa mkopo, Brentford ikionyesha nia ya kumtaka kinda huyo mwenye umri wa miaka 19. (Goal)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, anajiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza wakati huu akirejea kuichezea Tottenham kwa mara ya pili dhidi ya West Ham mwishoni mwa wiki ijayo. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 34, anasema alikaribia kutua ligi ya Serie A, wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari na dirisha kubwa lililofungwa wiki iliyopita. (RMC Sport, via Football London)

Frederic Guilbert

Manchester City wana matumaini Pep Guardiola atasaini mkataba mpya, lakini watatafuta mrithi wake iwapo meneja huyo ataonyesha dalili za kutaka kuondoka. (Telegraph)

Kiungo wa Hispania Dani Ceballos, 24, anasema alikuwa na shauku ya kurejea kwa mkopo Arsenal licha ya Real Madrid kumtaka kusubiri kwa mwezi mmoja. (Marca)

Kiungo wa Kiingereza Jack Wilshere, 28, anataka kuchezea klabu ya La Liga au Serie A baada ya kutemwa na West Ham. (Talksport)

Winga wa Kifaransa Allan Saint-Maximin, 23, anasema atakuwa na furaha kusalia Newcastle kwa muda mrefu- kama Magpies watafuata matamanio aliyonayo. (Newcastle Chronicle)

The post Aston Villa kuwauza wachezaji watatu kisa Josh King appeared first on Bongo5.com.