LIGI ya Mabingwa Barani Afrika imeendelea mwishoni mwa wiki hii,  ikiwa ni hatua ya nusu fainali kwa miamba ya soka  Afrika ya Kaskazini Morocco na Misri kutoana jasho vilivyo, ambapo National Al Ahly  wakiwa chini ya kocha mpya  Pitso Mosimane walikuwa ugenini kuvaana na Wydad Casablanca ya Morocco, na kuchomoza na ushindi wa magoli 2-0 na kujiweka katika mazingira mazuri katika mechi ya marudiano itakayochezwa Misri.


Pitso Mosimane ambaye ajiuzulu kuifundisha Mamelodi Sundowns ya Afrika ya Kusini mara baada ya kutwaa ubingwa,  ameonyesha ni kwa  jinsi gani anaweza kuipa taji  Al Ahly la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi huo wa ugenini wakisubiri kumaliza kazi nchini Misri.


Timu hiyo ambayo inaongoza kwa utajiri Afrika ilifunga magoli yake kupitia kwa Mohamed Magdy dakika ya nne na bao la pili likiwekwa kimiani na Ali Maaloul kwa mkwaji wa penati dakika ya 62.
Nusu fainali nyingine iliwashuhudia Raja Casablanca  wakiwakaribisha vigogo wengine,  Zamelek wa Misri ambapo walikubali kipigo cha goli 1-0  goli pekee la Zamelek likifugwa na Achraf Bencharki dakika 18 ambapo mechi za marudiano zitachezwa  tarehe 23 mwezi huu.


Kwa muktadha huo  huenda pakashuhudiwa fainali  kati ya  timu za Misri mechi, dabi ambayo inatajwa kuwa kali zaidi barani Afrika au timu za Morroco zitageuza kibao kwenye ardhi ya Farao?   Bado ni kitendawili ambacho kitateguliwa baada ya wiki moja.