Mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya kutengeneza pizza amekamatwa nchini Marekani baada ya mteja kupata wembe ndani ya mkate wa pizza alioununua, polisi imesema.

Duka la bidhaa mbalimbali – Saco Hannaford Supermarket, lililopo eneo la Maine liliifahamisha polisi baada ya wembe kupatikana katika mkate wa pizza wenye nembo ya Portland Pie ulionunuliwa katika duka hilo.

Nicholas Mitchell, ambaye ni mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya ‘It’ll Be Pizza’, ambayo ilitengeneza pizza hiyo, alikamatwa.

Picha ya video ya CCTV katika duka hilo ilikuwa imeonesha mwanaume akichezea bidhaa.

Haikubainika ni kwa sababu gani aliamua kufanya kitendo hicho.

Mshukiwa alikamatwa katika kituo cha polisi cha New Hampshire baada ya polisi kuweka rufaa.

Mteja aliyenunua mkate huo wa pizza kutoka Portland Pie na mkate wa jibini kutoka kampuni hiyo ya Portland Pie katika duka lolote la Hannaford kati ya Agosti 1 na 11 Oktoba wametakiwa kuirejesha dukani, limesema duka hilo.

“Baada ya kile kinachoaminiwa kuwa tukio la uchezeaji wenye nia mbaya uliohusisha vifaa vya chuma vilivyoingizwa kwenye bidhaa za Portland Pie, Hannaford imeondoa dukani bidhaa zote za Portland Pie na imesitisha kuleta tena bidhaa hizo dukani kwa muda usiojulikana,” Hannaford ilisema katika taarifa yake.

View this post on Instagram

——————————————————————————————————————————————————————————–Mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya kutengeneza pizza amekamatwa nchini Marekani baada ya mteja kupata wembe ndani ya mkate wa pizza alioununua, polisi imesema. Duka la bidhaa mbalimbali – Saco Hannaford Supermarket, lililopo eneo la Maine liliifahamisha polisi baada ya wembe kupatikana katika mkate wa pizza wenye nembo ya Portland Pie ulionunuliwa katika duka hilo. Nicholas Mitchell, ambaye ni mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya 'It'll Be Pizza', ambayo ilitengeneza pizza hiyo, alikamatwa. Picha ya video ya CCTV katika duka hilo ilikuwa imeonesha mwanaume akichezea bidhaa. Haikubainika ni kwa sababu gani aliamua kufanya kitendo hicho. Mshukiwa alikamatwa katika kituo cha polisi cha New Hampshire baada ya polisi kuweka rufaa. Mteja aliyenunua mkate huo wa pizza kutoka Portland Pie na mkate wa jibini kutoka kampuni hiyo ya Portland Pie katika duka lolote la Hannaford kati ya Agosti 1 na 11 Oktoba wametakiwa kuirejesha dukani, limesema duka hilo. "Baada ya kile kinachoaminiwa kuwa tukio la uchezeaji wenye nia mbaya uliohusisha vifaa vya chuma vilivyoingizwa kwenye bidhaa za Portland Pie, Hannaford imeondoa dukani bidhaa zote za Portland Pie na imesitisha kuleta tena bidhaa hizo dukani kwa muda usiojulikana," Hannaford ilisema katika taarifa yake. ( Via The Story) Written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Akamatwa baada ya mteja kupata wembe katika Pizza (+Video) appeared first on Bongo5.com.