Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kupita CCM, Dkt John Magufuli leo akiwa jijini Mbeya ameendelea na mikutano ya kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena.


Akiwa Jijini humo Dkt. Magufuli amesema endapo atachaguliwa tena, serikali atakayoiunda imedhamiria kulifanya jiji la mbeya kuwa lango kuu la utalii kwa mikoa ya ukanda wa Nyanda za Juu Kusini kwa kukamilisha upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songwe.


"Kwenye miaka 5 ijayo tutahakikisha tunakamilisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Songwe ili kufikia lengo la kufanya Mbeya kuwa lango kuu la utalii kwenye ukannda huu", amesema Dkt. Magufuli.


"Wakati Profesa Mwandosya anaanza kujenga huu uwanja wapo walioanza kulaumu anajipendelea kwa sababu anatoka Mbeya. Hyo ndiyo dhana fupi ya watu wasiofikiria mazuri", ameomngeza.