Afisa wa polisi wa ngazi ya juu nchini Afrika Kusini amekamatwa Jumatatu asubuhi,kufuatia tuhuma za ufisadi kwa mujibu wa kitengo cha upelelezi nchini humo.

Afisa huyo, naibu kamishena wa polisi ambaye jina lake limebanwa ni wa hivi punde kukamatwa kuhusiana na zabuni ya mamilioni ya fedha za kununua vifaa vya dhararu.

Kamishena wa kitaifa wa polisi, Khomotso Phahlane, ni miongoni mwa wale waliohusishwa na kesi hiyo. Hata hivyo amepinga tuhuma dhidi yake.

Maafisa wengine wa ngazi ya juu wameshitakiwa kwa tuhuma za ufisadi, ubadhirifu wa fedha, wizi na utakatishaji.

Imeelezwa kuwa Bei ya mkataba wa usambazaji wa vifaa ilikuwa Randi milioni 191 ($ 11.58 milioni) lakini ni Randi milioni 65 tu ($ 3.9 milioni) zilizolipwa kwa mtoa huduma, iliongeza.

Afisa huyo mwandamizi wa polisi anatuhumiwa kwa kusaidia uhalifu huo.

Wengine 11, wakiwemo maafisa wa polisi na raia, pia wamekamatwa katika kesi hiyo. Miongoni mwa hao ni kamishna wa zamani Khomotso Phahlane, ambaye amekanusha makosa yoyote.

Afrika Kusini imeongeza vita vyake dhidi ya ufisadi katika siku za hivi karibuni.

Naibu huyo wa kamishena wa polisi anatarajiwa kufunguliwa mashitaka leo Jumatatu.

Chanzo BBC.

The post Afisa mkubwa wa polisi akamatwa Afrika Kusini kwa tuhuma za ufisadi appeared first on Bongo5.com.