Lulu Diva ambae ameongea na simu kwa tabu amethibisha taarifa hizo kwa kusema ‘Ni kweli Millard tumepata ajali Chalinze, tulikua tunaendeshwa, mimi nimeumia kichwani nimevimba ila Belle 9 kaumia zaidi jamani amewaishwa Hospitali, @bongelanyau kaumia ila kiasi... mimi niko Polisi kuchukua Pf3 kisha nimfate @belle9tz Hospitali” @luludivatz
“Sijui chanzo ni nini maana wakati ajali inatokea nilikua nimelala nikaja kushtukia gari imeacha barabara na kupinduka, Belle 9 anaonekana ameumia mgongo na kichwani” - Lulu Diva.