"Tunapanga kuzindua chanjo ya (Covid-19) katika miezi ya kwanza ya mwaka (2021)," amesema rais ErdoÄŸan.
Rais ErdoÄŸan ametoa tamko hilo baada ya mkutano wa baraza la mawaziri.
Akisisitiza kuwa hatua mpya imeanza katika vita dhidi ya corona, ErdoÄŸan amesema kuwa wameanzisha mikakati mpya kulingana na uzoefu.
"Kati ya majaribio 8 ya maendeleo ya chanjo, majaribio 2 ya wanyama yamekamilishwa vyema."
"Tunapanga kuanza kutumia (chanjo) katika miezi ya kwanza ya mwaka (2021)"
"Uturuki ni kati ya nchi ulimwenguni ambazo zimesifiwa kwahuduma zinazopewa kwa wagonjwa toka mwanzo mwa janga hili.", alisema Erdogan, akikumbushia kuwa hatua muhimu zilichukuliwa ndani ya nchi hiyo.
"Kuchukua tahadhari hakumaanishi kumpa mtu shida, lakini ni njia kulinda afya za watu wetu wote." alimalizia kiongozi huyo.