Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ambao walikuwa chini ya lebo ya @officialalikiba @kingsmusicrecords ambao ni @officialcheed na @officialkilly_tz wametambulishwa rasmi kwenye lebo ya @kondegang iliyopo chini ya @harmonize_tz

kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram, wasanii hao wapya wa Konde Gang wametanagza kujiunga na lebo hiyo  huku wakimshukuru boss wao wa zamani Alikiba kwa kuwaonyesha njia na kuwaamini kufanya nao kazi.

ameandika Cheed na Killy kuwa :-

Habari Za Muda huu Ndugu Zangu …!!! Nianze Kwa Kuwashukuru Nyinyi Wote ambao Mmekuwa Na Mchango Mkubwa Sanaa Katika Safari Yangu Ya Mziki..!!! Mmekuwa Namimi Bega Kwa Bega Ninapo Nashukuru Sana Kwakweli Upendo wenu Wadhati Na Unamaanisha.. Kilakitu Kwangu ….!!!! Shukrani Za Dhati Zimuendee Kaka Yangu Kipenzi AllyKiba Natambua..!! Na Nitaendelea Kuuheshimu Mchango Wako Milele Yote Ulijitoa Kuhakikisha Watanzania Wananifahamu Kwa Kiasi Mpaka Pale Mungu Alipo Tuamuru Kupitia Njia Nyingine Katika Safari Hii Ya Utafutaji Wa Riziki. Leo Nipo Mbele Yenu Zaidi ni Kuwashuku Kwa Kuwa Sambamba Nami Lakini Pia Kuwataarifu Rasmi kwamba Kijana Wako Nimejiunga Na Kampuni Ya Uzalishaji Na Usimamizi Wa Muziki Tanzania KONDE MUSIC WORLDWIDE @KONDEGANG hii ni faraja Kubwa Kwangu na Sio Faraja Tuu bali Nitumaini Jipya kama Kijana wa Kitanzania Kupata Nafasi Ya Kufanya Kazi kwa Ukaribu na Wasanii Wenzangu @HARMONIZE_TZ & @IBRAAH_TZ @Youngskells Nawengine Natambua Kuna Wengi hata Wenye Kipaji Kunizidi Wangetamani Kuwepo Hapa Lakini Naamini Kilakitu Huja Kwa Wakati…!! Naamini Kwa Pamoja Tutashirikiana Ili kuzitunza Familia Zetu Masikini Nimalize kwa Kushukuru Uongozi Wa KONDE MUSIC WORLDWIDE Kwa Nafasi hii Ya Peke pia Niwaombe Ndugu Zangu Muendelee Kutuunga Mkono Na Mungu atawabariki Sana …!!! #KONDEGANG4EVERYBODY

Cheed na Killy walijitoa Kings Music mwezi Aprili, hivyo wataungana na wasanii kama Ibrah Tz, Young Skales kwenye lebo ya Konde Gang ambayo inasimamiwa na Harmonize.

View this post on Instagram

Habari Za Muda huu Ndugu Zangu …!!! Nianze Kwa Kuwashukuru Nyinyi Wote ambao Mmekuwa Na Mchango Mkubwa Sanaa Katika Safari Yangu Ya Mziki..!!! Mmekuwa Namimi Bega Kwa Bega Ninapo Nashukuru Sana Kwakweli Upendo wenu Wadhati Na Unamaanisha.. Kilakitu Kwangu ….!!!! Shukrani Za Dhati Zimuendee Kaka Yangu Kipenzi AllyKiba Natambua..!! Na Nitaendelea Kuuheshimu Mchango Wako Milele Yote Ulijitoa Kuhakikisha Watanzania Wananifahamu Kwa Kiasi Mpaka Pale Mungu Alipo Tuamuru Kupitia Njia Nyingine Katika Safari Hii Ya Utafutaji Wa Riziki. Leo Nipo Mbele Yenu Zaidi ni Kuwashuku Kwa Kuwa Sambamba Nami Lakini Pia Kuwataarifu Rasmi kwamba Kijana Wako Nimejiunga Na Kampuni Ya Uzalishaji Na Usimamizi Wa Muziki Tanzania KONDE MUSIC WORLDWIDE @KONDEGANG hii ni faraja Kubwa Kwangu na Sio Faraja Tuu bali Nitumaini Jipya kama Kijana wa Kitanzania Kupata Nafasi Ya Kufanya Kazi kwa Ukaribu na Wasanii Wenzangu @HARMONIZE_TZ & @IBRAAH_TZ @Youngskells Nawengine Natambua Kuna Wengi hata Wenye Kipaji Kunizidi Wangetamani Kuwepo Hapa Lakini Naamini Kilakitu Huja Kwa Wakati…!! Naamini Kwa Pamoja Tutashirikiana Ili kuzitunza Familia Zetu Masikini Nimalize kwa Kushukuru Uongozi Wa KONDE MUSIC WORLDWIDE Kwa Nafasi hii Ya Peke pia Niwaombe Ndugu Zangu Muendelee Kutuunga Mkono Na Mungu atawabariki Sana …!!! #KONDEGANG4EVERYBODY

A post shared by CHEED (@officialcheed) on

View this post on Instagram

Habari za muda huu ndugu zangu;Naitwa Ally Killy Omary Almaarufu kama “KILLY” ni msanii wa bongo flavour as we know, nianze kuwashkuru nyinyi nyote ambao mmekuwa na mchango mkubwa sana katika safari yangu ya mziki mmekuwa na mimi bega kwa bega kwa bega pale nnapopatia na hata nnapokosea pia kama wanadamu wengine kwakweli upendo wenu ni wa dhati na unamaanisha kila kitu kwangu.Lakini pia siwezi kumsahau kaka angu aliyenilea,akaniamini na kunishika mkono na kuniaminisha zaidi kwa watanzania hasa kwa mashabiki wa bongoflavour na kwa wadau wote waliopo kwenye tasnia yetu hii na kunionyesha njia katika kipindi chote tulichokuwa pamoja,kaka angu #ALIKIBA Mungu akuzidishie na mchango wako ntaendelea kuuheshimu milele.Napenda kuwataarifu mashabiki zangu na watu wote wanaosupport kazi zangu kiujumla tangu hapo awali mpaka hapa nilipofikia naamini bila mioyo yenu thabit na yenye upendo nisingekuwa Killy huyu wa leo hii ambae nawajulisha kuwa kijana wako nimejiunga rasmi na kampuni ya uzalishaji na usimamizi wa muziki Tanzania @kondegang #KONDEMUSICWORLDWIDE hii ni faraja kwangu na sio faraja tu bali ni tumaini jingine nikiwa kama kijana wa kitanzania kupata nafasi ya kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na wasanii wenzangu @harmonize_tz @ibraah_tz @youngskales na wengine natambua kuna wengi hata wenye kunizidi wangetamani kuwepo hapa lakini naamini kila kitu huja kwa wakati naamini kwa pamoja tutashirikiana katika safari ya kusaka mkate wa kila siku ili kuzitunza familia zetu za kimaskini.Nimalize kwa kuushkuru uongozi mzima wa @kondegang na C.E.O mwenyewe @harmonize_tz kwa kuthamini kipaji changu nilicho nacho ambacho Mwenyezi Mungu amenijalia kwa namna moja ama nyingine na kwa kunipokea kwa mikono miwili bila kujali pengine labda kama kuna vitu ambavyo vingeweza kusababishia wao kukataa kunipokea au kukataa hata pengine kuniskiliza walau hata kidogo lakini all in all Mungu aliwatia nguvu na moyo wa kuweza kuniskiliza na kunifkiria kwa upana zaidi jinsi gani wataweza kuendeleza kipaji changu so nawashkuru sana na Mungu awazidishie zaidi na zaidi. #KILLY #KONDEGANG4EVERYBODY

A post shared by Killy (@officialkilly_tz) on

The post Ujumbe wa Cheed na Killy kwa Alikiba baada ya kutambulishwa Konde Gang na harmonize appeared first on Bongo5.com.