Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeikabidhi ofisi ya taifa ya Mashitaka chini ya DPP jengo lililokuwa likitumiwa na mamlaka hiyo kanda ya Kigosi lililopo wilayani kahama mkoani Shinyanga baada ya mapori waliyokuwa wakiyasimamia kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi za taifa ambapo jengo hilo litatumika kuendesha kesi za jinai ikiwa ni mkakakti wa serikali wa kupunguza Msongamano wa maabusu na waafungwa katika Magereza nchini
Akizugumza Jana baada ya Makabidhiano ya jengo hilo Kaimu Kamishina wa uhifadhi nchini Mabula Nyanda amesema kuwa kutokana na uhusiano uliopo kati ya ofisi yake na ofisi DPP wamekuwa wakishirikiana katika masuala ya uendeshaji wa kesi za makosa yaliyokuwa yakihusika na rasimali za wanyama pori ambapo wameamua kuwapatia jengo hilo kwa muda ili waweze kusaidia jamii katika kesi mbalimbali
“Kama mnavyojua moja ya kazi muhimu sana katika taasisi hizi ni ulinzi wa rasimali za wanayamapori ambazo ni kazi za hima sheria kama mnavyojua ziko nne kwanza kuna operation, ukusanyaji wa taarifa, uendeshaji wa mashitaka na upelelezi hizi zote ni zinahusika na mashitaka,”amesema Kaimu Kamishina Nyanda
Amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana sana na ofisi ya taifa ya mashitaka katika kesi zote ikiwemo zinazohusu usimamizi wa rasilimali za wanyamapori ambapo DPP amekuwa msaada mkubwa wa kupambana na uharifu kwenye ujangili,mifugo na uvamizi wa mapori ya akiba hivyo tumeona umuhimu wa kuwapa jingo hili.
“Sisi tulikuwa tunatumia ofisi hii ya Kanda ya kigosi toka hapa Kahama baadae serikali ikapandisha hadhi mapori hayo toka pori la akiba hadi kuwa hifadhi, hivyo tukaaamua kupisha na tulikuwa na mpango wa kuwekeza mradi, ndipo tukapokea maombi toka kwa mdau wetu muhimu ofisi ya DPP wakitaka tuwapatie kwa ajili ya kufungua ofisi ya taifa ya mashitaka ya wilaya ya kahama nasi hatukuwa na shida tukaamua kumpa kwa muda kwa ajili ya utekeleza wa kazi zake za kuhudumia wananchi”
Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini Bishwalo Mganga amesema kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu walikuwa wakisafiri kwenda kupata huduma mkoani Shinyanga hali amabyo ilikuwa inachangia kuchelewa kutolewa kwa maamuzi hivyo kusogezwa kwa huduma hiyo wilayani kahama itasaidia kupungza adha ya kusafiri umbali mrefu.
“Tumeamua kufungua ofisi hapa kwa sababu gereza la kahama linapokea watu wengi kwa sababu linapokea kutoka wilaya jirani za Mbogwe na Bukombe zilizoko Mkoani Geita hivyo kuna kesi amabazo hazina ulazima sana wakili wa serikali atazichuja na kuzitoleea maamuzi nay ale yanayoshindikana yanakuja kwetu”
Biswalo amesema kuwa uwepo wa ofisi hiyo wilayani kahama utasaidia kupunguza Msonagamano ulioko kwenye gereza hilo pamoja na kuhakikisha kwamba kesi zinaendeshwa mapema na kwa mujibu wa sheria huku ofisi yake ikiendelea na mkakati wa kuwa na majengo ya ofisi zake
Naibu Katibu Mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju amesema kuwa nchi haiwezi kuwa na amani pasipo uwepo wa ofisi ya Taifa ya mashitaka hivyo uwepo wake ni muhimu sana katika kuhakikisha amani inadumu huku akibainisha kuwa mara baada ya kutembelea gereza la kahama ni jambo jema lililofanywa na DPP la kuomba kupewa jingo kwa ajili ya kuanzisha ofisi hiyo.
“Ni vema ushirikiano huu ukaendelezwa kati ya TAWA na DPP ili kuhakikisha Ulinzi wa Rasilimali za nchi zinaendelea kulindwa na kutunzwa kwa mujibu wa sheria za nchi nimefurahi sana kwa hili lililofanyika leo kuamua kuwapa jengo hili ofisi ya DPP nanyi hakikisheni mnalitunza ili hata mkiondoka libaki katika ubora wake”
Naye katibu tawala wa wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya amesema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina idadi kubwa ya wakazi takribani milioi moja hali inayochangia kuongeza vitendo vya uharifu na ongezeko la makosa ya jinai hivyo uwepo wa Ofisi ya DPP utasiadia kuondoa kero kwa wananchi ikiwemo ucheleweshwaji wa kesi.
Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi Elizabeth Mbezi amesema iwapo itaanza kufanya kazi ofisi ya mshitaka ya taifa itasiadia kupunguza kesi za watuhumiwa ambao hawana ulazima sana wa kukaa gerezani pamoja kupunguza Msongamano wa Mahabusu ndni ya gereza
“Kwa sababu Gereza letu la Kahama linapokea watuhumiwa toka halmashauri tatu wa wilaya hii pamoja na wilaya jirani za Mbogwe na Bukombe ambao hutumia gereza hilo kwa hiyo ifsis hii itasiadia kurahisisha mahabusu ambao si lazima kwenda gerezani kesi zao zikaishia nje”amesema Mbezi