Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri, EFA, Ahmed Shobir amesema kombe la AFCON limepotea katika makao makuu ya Shirikisho hilo.


Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON lilikuwa limehifadhiwa Misri baada ya timu ya Pharaohs kushinda kwa mara tatu mfululizo tangu mwaka 2006 hadi 2010.

Ameongeza kuwa “EFA ilimeanza kutafuta namna ya kupata kombe lingine linaloendana na hilo kwa ajili ya kuwekwe kweney sehemu au jumba la kumbukumbu la EFA,” Shobier alisema.

“Hata hivyo, EFA ilishangaa kupata taarifa kwamba kombe la AFCON limepotea na ingawa tumeamua kuacha uchunguzi wa haraka”

Watendaji wa Shirikisho hilo wamedai ya kuwa kombe hilo lilikuwa limehifadhiwa kwa nahodha wa timu ya taifa, Ahmed Hassan. Hassan ambaye naye amekanusha hilo na kusema alikaa nalo kwa siku moja baada ya kushinda na alikambidhi tangu mwaka 2011.

 

The post Shirikisho la soka Misri: Kombe la AFCON lililoibiwa lilikuwa kwa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Misri appeared first on Bongo5.com.