Rais wa Marekani Donald trump amezuru Kenosha, Wisconsin, kuunga mkono utekelezaji wa sheria baada ya kitendo cha polisi kumpiga risasi mwanaume mweusi kusababisha maandamano.
Rais Trump wa chama cha Republican amelaumu uvamizi wa ndani na uharibifu ulitotekelezwa mjini humo.
Kenosha imeshuhudia siku kadhaa za maandamano baada ya polisi kumpiga risasi mwanaume mweusi mamno Agosti 23 na kumsababishia kupooza.
Kura za maoni zinaonesha kwamba Bwana Trump amepunguza pengo lililokuwa kati yake na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden kabla ya uchaguzi wa Novemba.
Rais akiendelea kusisitizia utekelezaji wa sheria na utaratibu, Bwana Biden amemshutumu Trump kwa kuendeleza mgawanyiko kwa misingi ya ubaguzi.
“Moto unawaka na tuna rais ambae anauchochea badala ya kuuzima,” aliyekuwa makamu rais alisema hivyo kabla ya mkutano wake unaotarajiwa kufanya Jumanne.
Trump Alisema nini Kenosha?
Rais alitembelea maeneo yaliyoharibiwa na waandamanaji, ikiwemo duka la samani lililotiwa moto wakati wa maandamano.
“Haya si matendo ya maandamano ya amani, bali ni ugaidi wa ndani,” aliwaambia viongozi wa biashara katika mkutano wa pamoja uliofanyika kwenye mazoezi ya viungo ya shule ya sekondari.
Rais alionesha huruma kidogo kwa walioumia wakati wa makabiliano na polisi, akisema anahisi vibaya kwa yeyote yule anayepitia hayo. Lakini alisema haamini kwamba kuna mfumo wa kibaguzi katika utekelezaji wa sheria.
Bwana Trump alisema alituma jeshi la ulinzi wa Taifa huko Kenosha, ingawa lilipelekwa na gavana wa Wisconsin na kuungwa mkono na maafisa 200 wa serikali kulingana na agizo la rais.
Alisema utawala wake utatoa karibu dola milioni 4 kusaidia biashara za mji wa Kenosha ambazo zimeharibiwa na vurugu na uporoji huku dola milioni 1 ikitengewa mji huo kwa utekelezaji wa sheria.
Waandamanaji hao wameshutumu waandamanaji kutoka nje ya mji walioteka nyara maandamano yao. mwishoni mwa juma lililopita, polisi ilisema washukiwa 105 kati a 175 waliokamatwa wakati wa aandamano walikuwa wanatoka nje ya mji.
Kwanini Trump hakukutana na familia ya Blake?
Rais alisema hakukutana na familia ya Blake kwasababu walitaka mawikili wawepo.
Bwana Trump badala yake alisema anafuraha kujumuika na wahubiri wa mama yake Blake kwenye meza ya mazungumzo.
Mhubiri huyo kwa jina Sharon alisema: “Nafikiri ni muhimu kuwa na watu weusi kwenye meza ya mazungumzo kusaidia kutatua tatizo.”
Awali, katika mahojiano na CNN, baba yake bwana Blake, ambaye pia anajulikana kama Jacob Blake alisema maisha ya toto wake ni muhimu kuliko kukutana na Rais.
“Mimi siingii kwenye siasa. Muhimu ni mtoto wangu. Hakuna uhusiano wowote na kupiga picha,” alisema.
Baba yake Blake alisema kijana wake bado ni mlemavu kuanzia kwenye kiuno kwenda chini, “akipigania maisha yake”.
Afisa wa polisi alimpiga risasi Blake mara saba mgongoni alipokuwa akimkamata wakati mwathirika anaingia kwenye gari kulikokuwa na watoto wake watatu ambao walikuwa wameketi.
Ziara ya Bwana Trump mji wa Kenosha ilifanyika licha ya wito kutoka kwa meya wa Democratic na gavana wa kufuta ziara hiyo.
Mwishoni mwa juma lililopita, meya wa Kenosha John Antaramian alisema huu sio wakati muafaka kwa Bwana Trump kuzuru eneo hilo.
“Kiuhalisia, kwa mtazamo wetu, tungependelea asitembelee eneo kwa wakati huu,” alizunguma katika kituo cha redio cha taifa.
Gavana wa Wisconsin Tony Evers wa chama cha Democratic also pia alionya dhidi ya ziara hiyo, akisema kwamba “huenda ikawa kikwazo cha uponyaji”.
The post Rais Trump aelezwa kuwa upande wa Polisi, ayaita maandamano ya watu weusi ya kigaidi (+Video) appeared first on Bongo5.com.