Lulu amethibisha na kusema; “Ni kweli tumepata ajali, tulikuwa tunaendeshwa. Mimi nimeumia kichwani, nimevimba ila Belle 9 ameumia zaidi, amewahishwa hospitali kwa matibabu. Bonge la Nyau ameumia kiasi. Kwa sasa nipo polisi kuchukua PF3 kisha nimfuate Belle 9 hospitali.
“Sijui chanzo ni nini maana wakati ajali inatokea nilikuwa nimelala nikaja kushtukia gari imeacha barabara na kupinduka. Belle 9 anaonekana ameumia mgongo na kichwani,” Lulu Diva.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bonge la Nyau amesema, “Mwenyezi Mungu ametunusuru kwenye ajali mbaya iliyotokea mida hii tukiwa njian maeneo ya Ubena Chalinze.”