Hatimaye Nahodha na Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal ya England, Pierre Emerick Aubameyang amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake makuu Kaskazini mwa jijini London.
Aubameyang mwenye miaka 31 ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal hadi mwaka 2023, baada ya kusaini dili hilo ambalo litamfanya awe analipwa mshahara wa Pauni 250,000 kwa juma.
Aubameyang amesema:”Mwisho wa siku nimesaini bonge moja ya saini, nina furaha kuwa ndani ya Arsenal. Hapa ni nyumbani na ni furaha kwangu.
“Siku ya leo (jana) ni kubwa kwangu na ninahitaji kuwa Legend ndani ya Arsenal na nitakapoondoka niache alama. Ni muda wangu wa kazi na nitapambana.”
Kabla ya kusaini mkataba mpya jana Septemba 15, Aubameyang alihusishwa na taarifa za kuwaniwa na klabu za ndani na nje ya England, huku manguli wa Ligi ya nchini Hispania Real Madrid na FC Barcelona walikua wakitajwa mno na vyombo vya habari.