Alexis Sanchez ametoa ya moyoni kuhusu maisha yake aliyopitia ndani ya Manchester United wakati alipotua akitokea Arsenal mwaka 2018.

Alexis Sanchez has lifted the lid on his time at Manchester United with some shocking truths

Nyota huyo wa kimataifa kutoka Chile amedai kuwa mwenyewe aliomba kurudi katika klabu aliyotoka akimaanisha Arsenal baada ya siku ya kwanza tu ya mazoezi ndani ya Manchester United.

Sanchez alivumilia kwa kuendelea kukaa Old Trafford, licha ya kuwa Mashetani hao Wekundu walikuwa wakimlipa paundi 560,000 kwa wiki. Kutokana na kukuta asichokitarajia nyota huyo alijikuta akifunga mjula  ya magoli matano (5) pekee kwenye michezo yake 45 aliyocheza kabla ua kutimkia Inter Milan kwa mkopo msimu wa 2019-20.

The Chilean revealed he asked his agent to move him back to Arsenal after one training session

Mchezaji huyo wa miaka 31, akizungumza kwenye video fupi kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ameonekana kuwashangaza wengi, na kuthibitisha Manchester City kuwa walimuhitaji lakini dakika za mwisho na kujikuta akijiunga na United na kukiri kwamba aliuliza kama anaweza kurudi zake Arsenal baada ya siku moja tu akiwa chini ya Jose Mourinho.

“Nataka kuwaambia juu ya kipindi changu ndani ya United, kuhusu mambo mengi ambayo yalisemwa na ambayo yalinifanya nionekane mbaya. Nilipata fursa ya kwenda United, kilikuwa ni kitu kizuri kwangu, kwa sababu nilipokuwa mtoto nilipenda kilabu hiyo sana.”- Sanchez

“Niliishia kusaini bila kuwa na taarifa za kutosha juu ya kile kinachotokea ninapo elekea. Siku za kwanza ambazo nilikuwa na wenzangu, wakati mwingine kuna mambo ambayo huwezi kuyajua hadi utakapofika.”

”Siku yangu ya kwanza tu ya mazoezi niligundua vitu vingi. Nilirudi nyumbani na nikamwambia mwakilishi wangu, Je! Mkataba hauwezi kusitishwa na kurudi Arsenal?”

”Walianza kucheka na niliwaambia kuwa kuna kitu hakikuwa sawa kwangu, tayari ilikuwa imesainiwa.” Sanchez alikumbuka wakati mmoja akiwa Manchester United ambapo aliachwa na Mourinho nje ya kikosi cha siku hiyo ya mechi yao dhidi ya West Ham mnamo Septemba 2018.

Kutofanya vizuri kwa Sanchez Man Unite kuliwashangaza wengi sana hasa kutokana kuwa moja ya washambuliaji bora kabisa England akiwa Arsenal.

Sanchez was signed by Manchester United in 2018 and earned around £560,000-a-week

Sanchez aliongeza ”Mechi na West Ham sikuchaguliwa kikosini, hiyo haikuwahi kutokea kwangu mimi kama mchezaji, ilinisumbua sana na nikasema haiwezekani.”

”Nikitoka kuwa mmoja wa wachezaji bora ndani ya Premier League, mpaka kutocheza katika miezi mitano. Nilirudi nyumbani kwangu na nilikuwa na huzuni. Siku iliyofuata nilifanya mazoezi mara mbili ya kawaida kwa sababu naipenda kile ninachokifanya.”

Manchester United ilipoteza mbele ya West Ham kwa magoli 3-1 na Mourinho kutimuliwa na miezi michache baadaye, Sanchez alitumia nafasi hiyo kuzungumza na Ole Gunnar Solskjaer ambaye alichukua nafasi ya Mourinho, kuhusu kuomba kuondoka.

Sanchez akaongeza ”Kisha kocha mpya akawasili na ndipo nilipoamua kuongea naye, nikamwambia nahitaji kuondoka na kuna fursa ya kwenda Inter. Alinijibu sawa hakuna tatizo.”

Winga huyo alifunga jumla ya magoli 80 kwenye michezo yake 166 aliyocheza Arsenal kabla ya kuelekea Old Trafford mwezi Januari 2018.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

The post Nilitaka kurudi Arsenal siku ya kwanza tu Manchester United – Sanchez afunguka mazito appeared first on Bongo5.com.