Kampuni ya ndege nchini Kenya, Kenya Airways (KQ) imeanza rasmi safari zake nchini Tanzania baada ya taifa hilo kuondoa marufuku ya safari za ndege za Kenya iliyokuwa imeiweka mwezi uliopita, kulingana na taarifa ya Mamlaka ya safari za anga nchini Tanzania TCAA.
Ndege hiyo ya Kenya imeanza rasmi safari mara mbili kutoka Dar es Salaam mpaka Nairobi na mara tatu kwa wiki kuelekea Zanzibar.
Hatua hii ya kufunguliwa kwa ndege za Kenya kwenda nchini Tanzania imekuja baada ya Kenya kuondoa sharti la kuwaweka karantini kwa muda wa siku 14 Watanzania wanaoingia nchini humo.
Kupitia ukurasa wao wa Twitter wamepost ujumbe huu:-
It was an honour for us to resume commercial passenger flights to the beautiful city of Dar-es-Salaam, Tanzania today. We are delighted to offer 14 flights weekly between Nairobi and Dar. Visit https://t.co/prAhdZfXNS to book your ticket! #KQClearForTakeOff @officialtcaa pic.twitter.com/LP2ylCfzgM
— Kenya Airways (@KenyaAirways) September 21, 2020
The post Ndege za Kenya Airways ‘ KQ ‘ zaanza safari za kila siku Tanzania – Video appeared first on Bongo5.com.