Mwanamke mmoja amekamatwa kwa kushukiwa ndiye aliyetuma barua yenye sumu kwenda kwa Rais wa Marekani, President Donald Trump.
Mtu huyo alitiwa mbaroni katika mpaka alipokuwa akiingia Marekani kupitia jimbo la New York akitokea Canada, mamlaka za usala zimesema.
Barua hiyo iligunduliwa katika kitengo cha ukaguzi wa vifurushi vya barua katika Ikulu ya White House mapema wiki hii , wanasema maafisa.
Walisema kuwa sumu hiyo iliyopatikana ndani ya bahasha ilitambuliwa kama ricin, sumu ambayo kwa kawaida hupatikana katika maharagwe.
Ricin hutengenezwa kwa kusindikwa kwa maharage ya castor . Ni sumu inayoua ambayo kama ikimezwa, kuivuta wakati wa kupumua au kuchomwa sindano yake , inaweza kusababisha kizunguzungu, kutapika, kuvuja damu ndani ya mwili na kusimamisha utendaji wa viungo vya ndani ya mwili.
Iwapo mtu atatumia sumu ya ricin, kifo chake kinaweza kutokea katika kipindi cha saa 36 na 72, kulingana na kiwango cha dozi iliyoingia mwilini mwake, kwa mujibu wa Kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuwia magonjwa (CDC).
The post Mbaroni kwa kumtumia barua ya sumu Rais Trump appeared first on Bongo5.com.