Marekani imetangaza kuwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vimeanza tena kutekelezwa na kuahidi kuwaadhibu wale watakaovikiuka, katika hatua ambayo inatishia Marekani kuendelea kutengwa na pia kuzusha mivutano ya kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema serikali yake inakaribisha vikwazo vyote vilivyokuwa vimewekwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kulingana na yeye, vikwazo hivyo vilianza kutekelezwa saa sita usiku wa kuamkia leo. Serikali ya Rais Donald Trump pia imeahidi kuliwekea vikwazo taifa lolote mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambalo halitatekeleza vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, hata ingawa ndiyo nchi pekee ulimwenguni inayoamini kuwa vimeanza tena kutekelezwa.
Trump huenda akatangaza hatua hizo wakati wa hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne wiki ijayo.
The post Marekani yadai vikwazo vya UN dhidi ya Iran vinatekelezwa upya appeared first on Bongo5.com.