Picha inayomuonesha mamba akiwabeba watoto wake mgongoni kwa kutumia mbinu isiokuwa ya kawaida inaendelea kuzua gumzo mitandaoni.
Picha hiyo ya kuvutia ilinaswana mpicha Dhritiman Mukherjee katika hifadhi ya Uttar Pradesh nchini india.
Miito imekuwa ikitolewa kupendekeza mpiga picha huyo apewe tuzo ya mwaka huu ya picha bora ya wanyhama pori.
“Ili kujiokoa watoto walilazimika kujishikilia katika eneo la kichwa cha mama na hata wengine kupanda mgongoni ili kuwa salama,” anasema.
Thuluthi tatu ya mamba hao wanapatikana katika hifadhi ya Uttar Pradesh, hali ambayo huenda ikawa jambo la muhimu kwa mamba wadogo kujilinda kwa njia isiokuwa ya kawaida wanapobebwa na mama zao.
Chanzo BBC.
The post Mamba aliyepata umaarufu India, baada ya kuonekana akiwapa ulinzi wa kipekee watoto wake appeared first on Bongo5.com.